Na John Walter -Babati
Baadhi ya
Wananchi katika Kata ya Ayalagaya (Dareda) katika wilaya ya Babati
mkoani Manyara wameshuhudia mnyama fisi akiwa amekufa barabarani baada
ya kugongwa na gari.
Baadhi
ya wananchi waliokuwa wanapita katika eneo hilo wamedai kuwa fisi huyo
amegongwa na gari usiku wa kuamkia leo agosti 11 mwaka huu japo hawajui
ni gari gani.
Mwananchi
mmoja mkazi wa Gajal ambae hakutaja jina lake amesema eneo hilo lina
fisi wengi ambao hudhuru watu na mifugo haswa nyakati za usiku.
Taarifa
iliyotolewa mwaka 2020 na mtafiti wa Simba wa Ikolojia ya
Manyara-Tarangire Dr Bernard Kissui alisema kila siku mnyama mmoja
anagongwa na gari ambapo katika uchambuzi wao walibaini aina tofauti 50
hugongwa na magari wengi wakiwa ni wanyama wanaozaa (Mamalia) na
wanaotaga mayai.
Dr
Kissui alisema katika mwaka huo Wanyamapori 380 walikufa kwa kugongwa na
magari katika mapito ya wanyama, yanayopitiwa na barabara kuu ya
Arusha-Babati.
Mara
nyingi katika bara bara ya Babati-Singida wanyama wanaonekana kufa kwa
kugongwa ni Mbwa,na huwa ni nadra sana fisi kuonekana barabarani wakiwa
wamegongwa ukizingatia kuwa bara bara hiyo haina hifadhi ya
wanyamapori.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...