Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC imesaini mkataba wa miaka miwili na kampuni ya Kusambaza vifaa vya michezo Duniani MASITA SPORTS WEAR ya Nchini Uholanzi kwa ajili ya kusambaza vifaa vya timu kwa miaka miwili.

Makubaliano hayo yamefanyika jijini Dar Es Salaam leo chini ya Kampuni ya Level Up ambao ndio wawakilishi wenye hati miliki ya kusambaza vifaa vya MASITA kwa ukanda wa Africa Mashariki na Kati.

Katibu Mkuu wa KMC FC Mr Walter Harson amesema MASITA ni kampuni bora na wanategemea ubora zaidi utaongezeka baada ya kufanya kazi kwa msimu uliopita kwa kiwango kikubwa.

Awali wakisaini mkataba huo , Mkurugenzi Mtendaji wa Level Up Mr Daud Aboud amesema ni nafasi kubwa kwao  kufanya kazi na timu kubwa kama KMC FC na wana imani watashirikiana vizuri katika makubaliano hayo na hivyo kutimiza malengo ya kuhakikisha wanaleta vifaa bora vinavyotengenezwa na kampuni hiyo ya MASITA.


Mwenyekiti wa Timu ya KMC FC , Kheri Misinga wapili kulia , Mkurugenzi  Mtendaji wa Level Up, ndugu. Daudi Aboud watatu katikati wakiwa wameshika mkataba wa Makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya KMC FC uliosaniwa leo Jijini Dar es Salaam.

 

 Katibu wa KMC FC Walter Harison akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa  Level Up ,. Daud Aboud wakiwa wameshika Mkataba wa Makubaliano ya usambazaji wa vifaa vya michezo ya Timu ya KMC FC.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...