Na Mwandishi wetu
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imewataka Maafisa
Forodha wa TRA pamojana maafisa wa taasisi nyingine za Serikali kuhakikisha
kuwa wanahamasishamatumizi sahihi ya kisheria katika Vituo vya Huduma kwa
Pamoja Mpakani ili watumbalimbali wanaopita kupitia katika mipaka hiyo waweze
kuhamasika kutumianjia sahihi badala ya njia zisizo rasmi.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Naibu Kamishna wa TRA,
Bw. Msafiri Mbibowakati alipofanya ziara yake ya kikazi katika mpaka wa
Mutukula unaounganishanchi ya Tanzania na Uganda uliopo mkoani Kagera.
Bwana Mbibo amesema kwamba, lengo la kutaka kuwepo kwa
matumizi sahihi yasheria hizo katika maeneo ya mipakani ni kuzuia watumiaji
kutumia njia zisizorasmi ambazo zinaweza kuathiri takwimu za kiuchumi,
kuhatarisha usalama wanchi na pia uingizaji bidhaa mbazo hazina viwango ambazo
zitaumiza walaji wandani na zinaweza kuharibu mahusiano baina ya Tanzania na
nchi za jirani.
“Kuziingiza bidhaa ambazo hazina viwango nchini kwetu na
kupeleka bidhaaambazo hazina viwango kwa nchi ambazo ni majirani zetu
kutaharibu mahusianoyetu ya kibiashara pindi wakigundua tunaingiza nchini
mwao bidhaa za namnahiyo, hivyo lazima tusimamie vizuri sheria ili mambo haya
yasitokee”, alisema Mbibo.
Ameongeza kuwa, mpaka wa Mutukula kwa sasa ufanisi wake
unaoongezekamwaka hadi mwaka ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita wa 2020/2021ulipangiwa lengo la kukusanya shilingi bilioni 21 na
umefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 24 ambapo hiyo ni sawa ufanisi wa
utendaji wa asilimia 114ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2019/2021 malengo
yalikua ni kukusanyashilingi bilioni 18 na zikakusanywa shilingi bilioni 20
na zaidi.
“Mpaka huu ni wakutegemewa na unafanya vizuri zaidi, na
endapo tutazidikuongeza huduma au vitendea kazi katika mpaka huu basi
ufanisi huu wa sasa utazidi kuongezeka na tutaweza kuwahudumia wananchi wa
nchi jirani na Watanzania pia”
Aidha, amefafanua kuhusu magari yaliyopo mpakani hapo kwa
kusema kwamba,baadhi ya magari ambayo hayajakamilisha baadhi ya
taratibu ndogo ndogo wahusika huwa wanaitwa ili waweze kukamilisha taratibu
hizo ili waweze kulipa kodi zao na kuyaondoa, lakini pia kwa wale ambao
wameyatelekeza magari yao sheria inaitaka TRA kutangaza kwa muda fulani ili
wahusika wenyewe wajitokeze na kukamilisha taratibu za kiforodha na endapo hawajafanya
hivyo baada ya siku kadhaa kupita sheria inaitaka pia TRA iyaingize magari
hayo katika mnada ambao mtu atayevutiwa nayo aweze kuyanunua ili kodi ya Serikali
iweze kukombolewa.
“Mnada wa kuuza magari yaliyotelekezwa tunafanya kwa njia
ya mtandao (Online), hivyo mtu yeyote nchi nzima anaweza kushiriki
katika mnada, lakini kuna baadhi ya magari ya watu ambao ni wakorofi na wamekua
wakichezea chesisi namba za magari na kwa bahati nzuri sheria inamruhusu
Kamishna Mkuu wa TRA kuyatoa kwa namna anavyotaka yeye, basi sisi tunaweza
kuyagawa kwa taasisi nyingine za Serikali lakini hii huwa hatufanyi mara kwa
mara”, alisema Mbibo.
Naibu Kamishna Mkuu wa TRA yuko katika ziara ya kikazi
katika mikoa ya Kandaya ziwa na lengo la ziara hiyo ni kuona namna ya utendaji
kazi wa ofisi za TRAmipakani ikiwemo kusikiliza changamoto mbalimbali katika
ofisi hizo ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi wake na hatimaye makusanyo ya mapato
yazidi kuongezeka na kwenda kuleta maendeleo kwa Taifa.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Bw. Msafiri Mbibo akiongea na Watumishi wa TRA pamoja na watumishi wengine
wa baadhi ya taasisi za Serikali zinazofanya kazi pamoja katika Kituo
cha Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) cha Mutukula mkoani Kagera ambapo ni
mpakani mwa Tanzania na Uganda, kuhusu namna ya kushirikiana kwa pamoja na
kuwa na nidhamu katika kazi zao wanapokua mpakani hapo.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Bw. Msafiri Mbibo(wa pili kulia) akiongea na kutoa maagizo mbalimbali kwa
viongozi wa TRA katikaofisi ya TRA iliyopo eneo la Kyaka mkoani Kagera wakati
alipofanya ziara yake ya kikazi mkoani hapo kwa ajili ya kusikiliza changamoto
mbalimbali katika mpaka wa Tanzania na Uganda.
Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Bw. Msafiri Mbibo akimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Profesa
Faustin Kamuzora (kushoto) wakati alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo
la kufanya nae mazungumzo juu ya masuala mbalimbali ya kodi ikiwemo
namna bora ya kuboresha makusanyo ya mapato ya Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...