Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Mvumi Mkoani Dodoma  Livingstone Lusinde 'Kibajaji' amesema watu wanaodai kwamba wabunge hawalipi kodi, wanataka kupotosha umma.

Lusinde ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kauli ya aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, aliponukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wanapaswa kulipa kodi.

Amesema amesikitishwa kwani maneno hayo yamekuwa yakitolewa na viongozi wastaafu kisha kusambazwa katika mitandao ya kijamii.

“Leo nimeleta risiti za mshahara wangu ambazo zinaonyesha namna ambavyo wabunge tunakatwa fedha kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya taifa.

Itakuwa Nchi ya wapi ambayo watu wengine wanalipa kodi wengine hawalipi, naomba wananchi waelewe hata wabunge tunalipa kodi na tunakatwa katika mishahara yetu,” Amesema Lusinde.

Kuhusu tozo za miamala ya simu, Lusinde amebainisha kuwa wabunge hawakupanga kiwango cha tozo za miamala, lakini wao walipitisha sheria ya tozo na Waziri wa Fedha, akapanga viwango.

Amesema lawama nyingi zimekuwa zikiangukia kwa wabunge kuwa wameweka viwango vikubwa wakati wao hawahusiki kupanga viwango hivyo.

“Tusilaumiwe wabunge kuhusu tozo za mihamala kwa sababu hatukuweka kiwango bali tulipitisha sheria, ambapo tuliamini kuwa nchi itajengwa na kodi za wananchi hakuna mtu wa kuja kujenga,”Amesema.

Mbunge wa Jimbo la Mvumi Mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde 'Kibajaji' akizungumza na wandishi wa habari jijini Dodoma juu ya tuhuma za CAG mstaafu, Ludovick Utouh kuhusu Wabunge kutolipa Kodi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...