Na Munir Shemweta, KAHAMA
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameungana na viongozi wengine wa serikali katika mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hayati Elias Kwandikwa.
Mazishi hayo yamefanyika leo tarehe 9 Agosti 2021 katika kijiji cha Butibu kilichopo katika halmashauri ya Ushetu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro, Mawaziri, Wabunge na viongozi wa vyama vya Siasa.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hayati Elias Kwandikwa katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Butibu, Ushetu mkoani Shinyanga leo tarehe 9 Agosti 2021.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akisalimiana na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hayati Elias Kwandikwa yaliyofanyika kijiji cha Butibu, Ushetu mkoani Shinyanga leo tarehe 9 Agosti 2021.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akiwa na viongozi wengine wakati wa mazishi ya aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hayati Elias Kwandikwa yaliyofanyika kijiji cha Butibu, Ushetu mkoani Shinyanga leo tarehe 9 Agosti 2021.
( PICHA ZOTE NA MUNIR SHEMWETA WIZARA YA ARDHI)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...