MAKAMU wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema ni wakati wa serikali kushirikiana na nchi ya Msumbiji katika kuikuza sekta ya mafuta na gesi kwa ajili ya kuuinuwa uchumi wa Zanzibar kupitia sekta hiyo.

Mhe. Othman ameyasema hayo leo (Agosti 4) wakati akizungumza na Balozi Mdogo wa Msumbiji aliyepo Zanzibar, Balozi Agostinho Abaca Trinta, aliyefika ofisini kwake Migombani mjini Unguja kwa lengo la kujitambulisha.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Othman amesema Msumbiji ni nchi iliyopiga hatua katika sekta ya mafuta na gesi na hivyo pande hizi mbili zinaweza kubadilishana ujuzi na kuona namna ya kuikuza zaidi sekta hiyo.

Amesema mafuta na gesi ni miongoni mwa sekta ambayo kwa sasa Serikali ya Zanzibar inaipa kipaumbele kwa lengo la kuona inaongeza maeneo yatakayosaidia katika kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumzia suala la lugha ya Kiswahili, Mhe. Othman amesema ni wakati muafaka sasa kuifanya lugha ya kiswahili kuwa ni miongoni mwa lugha kuu barani Afrika na kwamba Msumbiji ina nafasi kubwa ya kuisambaza na kuieneza lugha hiyo kwa nchi za kusini mwa Afrika.

Aidha Mhe. Othman alimuelezea Balozi Agostino, fursa za kiutalii zilizopo Zanzibar ambazo zimekuwa ni chachu ya kuinua uchumi wa wananchi wa Zanzibar na nje ya Zanzibar waliowekeza katika sekta hiyo ambayo kwa sasa imekuwa ni sekta tegemezi kwa uchumi wa Zanzibar

"Kutokana na kukuwa kwa soko la utalii duniani, nchi hizi mbili ni vyema tukaangalia namna ya kushirikiana kupitia eneo hilo kwa lengo la kuona nchi zinakuza zaidi utalii wake duniani" alieleza Mhe. Othman

Naye Balozi Agostinho Abaca Trinta, akamuhakikishia Mhe. Othman kuwa nchi hiyo itaendelea kuwa pamoja na kukuza uhusiano wake na Zanzibar, ili kuona zinafikia maendeleo, pamoja na kueleza salamu za Rais wa nchi yake Mhe. Filipe Nyusi, zakusisitiza umoja na mshikamano kati yao na Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...