Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga takribani shilingi bilioni 41.87 kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini mkoani Rukwa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo Agosti 26, 2021 alipokuwa akizindua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili katika kijiji cha Lowe kata ya Lusaka Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Fedha hizo zitatekeleza miradi ya umeme kwenye vijiji 339 katika mkoa wa Rukwa.
Aidha, Dkt. Kalemani amesema kuwa, Serikali imetenga jumla ya shilingi Trilioni 1.24. kwa ajili ya kukamilisha utekelezaji wa miradi ya umeme Vijijini awamu ya tatu mzunguko wa pili hadi kufikia mwezi septemba mwaka 2022.
"Tanzania imefikia asilimia 86 ya usambazaji wa umeme katika vijiji na kuifanya kuwa ya kwanza Afrika kwa kusambaza umeme vijijini" alieleza Dkt. Kalemani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...