NA YEREMIAS NGERANGERA….NAMTUMBO.
TIMU ya Alkaida iliyopo Kijiji cha Namahoka kata ya ligera wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma imetamba na kusema kuwa timu hiyo ni bora kuliko timu zingine katika kata ya ligera.
Kocha wa timu hiyo Swadiku Abiru alisema maneno hayo mara baada ya kumalizika kwa dabi kati ya timu yake na timu ya komputa zote za kata hiyo na kudai kuwa Alkaida kwa sasa haina mpinzani kwani timu iliyokuwa tishio kwa kata ambayo ni komputa huifunga mara kwa mara.
Abiru alidai ndani ya miezi miwili timu hizo zimekutana katika dabi ya kushindania laki moja na katika fainali ya Zabri cup na kuigaragaza timu hiyo .
Abiru aliongeza kuwa kikosi chake cha timu ya Alkaida kimesheheni vijana wenye maarifa na ubunifu na wanaotekeleza maagizo ya kocha wakiwa uwanjani.
Kaimu mtendaji wa Kijiji cha Namahoka bwana Sixbert Milinga pamoja na mambo mengine aliiopongeza timu ya Alkaida kwa ushindi wa penati tano kwa saba na kumshinda mpinzani wake komputa .
Hata hivyo aliwapongeza komputa kwa kupambana lakini akawatia moyo kuwa asiyekubali kushindwa sio mshindani kwa kuwa hayo ndiyo matokeo na wanatakiwa kuyapokea.
Mdhamini wa dabi hiyo bwana Zablon Luena aliitaka timu iliyoshindwa kutokata tamaa na kuwahakikishia dabi zingine zijazo wajipange ili waweze kushinda.na katika dabi hiyo mdhamini alitoa shilingi elfu hamsini kwa timu iliyoshinda ya Alkaida na elfu ishirini kwa timu ya komputa.
Refarii wa dabi hiyo bwana Hekima Mango alionesha kuumudu mchezo kutoka mwanzo wa mchezo mpaka kumalizika kwa dabi hiyo kwa njia ya penati ambapo timu ya Alkaida iliifunga timu ya komputa kwa penati 7 kwa penati 5 .
Timu ya Alkaida kwa musimu huu 2021 imeonekana kuwa timu bora katika kata ya ligera baada ya kuzifunga timu za kata hiyo zilizokuwa hazifungiki siku za nyuma na timu hiyo.
Timu ya komputa
Timu ya Alkaida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...