MENEJA wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA} Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao cha Wafanyabiashara.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akifuatilia hoja mbalimbali katika kikao hicho.

Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia kikao hicho.

NA OSCAR ASSENGA, TANGA
MENEJA wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA} Mkoa wa Tanga Specioza Owure amesema mamlaka hiyo imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya asilimia 29.7 kwa mwaka 2020/2021.

Specioza aliyasema hayo wakati akitoa taarifa ya mapato kwa mwaka 2020/2021 na mipango mikakati ya ukusanyaji mapato waliojiwekea mwaka 2021/2022.

Alisema mamlaka hiyo mkoani Tanga imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh.Bilioni 154.5 wakati lengo lilikuwa ni kukusanya Sh.Bilioni 140.2 ambao ni utendaji wa asilimia 110 katika ya makusanyo hayo.

“Idara ya Kodi za ndani imekusanya zaidi ya Sh Bilioni 70.5 na Idara ya Forodha imefanikiwa kukusanya Bilioni 83.99 kwa mwaka 2020/2021 “Alisema

“Lakini kumekuwa na ongezeko la makusanyo kwa zaidi ya Bilioni 35.3 sawa na asilimia 29.7 ukilinganisha na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2019/20 ambapo mkoa ulikusanya Sh Bilioni 3.99 sawa na asilimia 2.85”Alisema Meneja Owure.

Alizitaja sababu ambazo ziliwawwezesha kufikia hatua hiyo ya kuvuka lengo kwa mwaka huo ni kuendelea kuwa na uhusiano mzuri kati yao na viongozi wa mkoa na wilaya zote pamoja na taasisi zote za Serikali na walipa kodi.

Meneja huyo alisema pia lengo la TRA Mkoa wa Tanga kwa mwaka 2021/2022 ni kukusanya zaidi ya Bilioni 180.88.

Hata hivyo alisema pia wana mikakati ya kuvuka lengo kwa mwaka huu,TRA imejipanga kufanya usajili wa wafanyabiashara wapya ambao hawamo kwenye wigo wa kodi.

“Pia tuna mkakati wa kuendelea kufuatilia na kudai madeni ya kodi kwa ukaribu na kwa mujibu wa sheria ili kuikomboa kizi hiyo.

Meneja huyo alisema pia wataendelea kufanya doria kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama mkoa ili kuweza kubaini na kuzuia biashara za magendo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...