Na Mwamvua Mwinyi,Mkuranga
KIONGOZI
wa mbio maalum za mwenge wa Uhuru ,LT.Josephine Mwambashi ameeleza ni
wajibu kuisaidia Serikali, kuzuia na kupambana na matumizi ya madawa ya
kulevya na kuwafichua wanaozalisha dawa za kulevya na wafanyabiashara
wakubwa wa madawa hayo .
Ameeleza,
jamii inapaswa kusaidia vyombo vya dola hususan polisi kuwabaini
wakulima wa bangi na wauzaji pamoja na wasafirishaji .
Akitembelea
mradi wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Kilimahewa ,Mwambashi
alielezea ,dawa za kulevya zina punguza nguvu kazi na kuhatarisha afya
ya watumiaji ambao hupata athari za kiakili na kupata magonjwa
yatokanayo na zinaa .
"Ni
jukumu letu kuisaidia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais
Samia Suluhu, kupambana na matumizi hayo,wanaozalisha dawa ya kulevya
kwasababu dawa ya kulevya kama mirungi,bangi zinazalishwa nchini kwetu
na baadhi ya wakulima wanatumia nafasi hizo kuzalisha mazao mchanganyiko
na bangi"
Nae
mkuu wa wilaya ya Mkuranga ,Hadija Nasir Ally alieleza ,amepokea mwenge
wa Uhuru ,agost 16 ukitokea wilaya ya Kibiti,ambapo ukiwa Mkuranga
mwenge huo utatembelea miradi 15 yenye thamani ya sh bilioni 21.1.
Kuhusiana
na mapambano dhidi ya dawa za kulevya ya wilaya , taarifa ilieleza
vijana 34 wanahudumiwa katika vituo vya kutolea huduma za afya .
Inasema
wilaya hiyo ,imefanikiwa kutoa elimu kufanya utambuzi wa waathirika wa
dawa za kulevya na kuwashawishi kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili
kujipatia kipato .
Muathirika
wa madawa ya kulevya Kudra Ibrahim alisema wapo wanne ,ambao wameamua
kutumia methadon kuachana na madawa ya kulevya na kujidunga.
Mwenge
huo ukiwa Mkuranga,pia umetembelea mradi wa uwezeshaji wa wanawake
kiuchumi ,kikundi cha wanawake cha wanawake cha Muungano Kilimahewa
Kaskazini chenye wanachama tisa, na wanafuga kuku wa asili.
Pamoja
na miradi hiyo, kuna mradi uliozinduliwa wa skimu ya maji Mkerezange
,Mkamba ambapo unatarajia kuhudumia Kijiji cha Kigoda na Mkerezange
vyenye wakazi 2,550.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...