Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KLABU ya Soka ya Yanga rasmi imetangaza kuachana na Makipa wake, Mtanzania Metacha Mnata na Mkenya Farouk Shikhalo ikiwa baada ya siku chache kutangaza usajili wa Golikipa mpya kutoka Mali, Djigui Diarra aliyekuwa akicheza Stade Maliƫn ya nchini humo.
Hatua ya Yanga SC kuachana na Wachezaji hao imetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Haji Mfikirwa wakati akifanya mahojiano Dar es Salaam na Kituo cha Runinga cha Azam TV.
Mfikirwa ameeleza kuwa wameendelea kufanya mazungumzo na Makipa hao wawili kwa ajili ya kukamilisha utaratibu wa kuachana vizuri katika Klabu hiyo.
Wakati huo huo Mfikirwa amethibitisha kuuzwa Kwa Mchezaji wao raia wa DR Congo, Tuisila Kisinda katika Klabu ya RS Berkane ya Morocco timu ambayo kwa sasa anafundisha aliyekuwa Kocha wake katika Klabu ya AS Vita Club, Florent Ibenge.
Mfikirwa amesema ofa iliyokuja mezani katika Klabu yao kutokea Berkane ni kubwa zaidi kwa maslahi ya Mchezaji na Klabu kwa ujumla hali inayopelekea faida kwa pende zote mbili.
“Tuisila bado tuna mkataba naye, tukimuuza akiwa na mkataba wake tutapa faida sisi kama Klabu, pia kuna vipengele vya ofa ambavyo vina maslahi mapana kwa Mchezaji mwenyewe binafsi.”Amesema Mfikirwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...