Na Lulu Mussa,KONGWA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ametoa rai kwa wakazi wa Kongwa kutoa msukumo wa dhati katika agenda ya mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti rafiki kwa mazingira.
Akiwa katika ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Kongwa Waziri Jafo ametoa rai hiyo leo kwa wana Kongwa na kuwataka kuunga mkono juhudi za Serikali za kuifanya Dodoma kuwa ya Kijani.
"Ndugu zangu Kampeni ya kukijanisha Dodoma ni endelevu, na Kongwa ni sehemu ya Mkoa wa Dodoma, natoa rai kwenu mpande miti kwa wingi, sambamba na kilimo cha Korosho kama zao la kimkakati" Jafo alisisitiza.
Amesema agenda ya mazingira iende sambamba na upandaji wa miti kwa kila kaya walau miti mitatu ikiwemo ya kivuli na matunda ili jamii iweze kunufaika nayo sambamba na hifadhi ya mazingira ikiwa ni pamoja na ulinzi endelevu wa miundombinu kama vile barabara na madaraja.
Amesema Kongwa ya sasa si sawa na Kongwa ya zamani kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu kama Ukataji wa miti kwa matumizi ya kuni na mkaa.
Waziri Jafo amesema Ofisi ya imezindua Kampeni Kabambe ya Kitaifa ya Uhifadhi na Usafi wa Mazingira kwa lengo la kunusuru taifa na majanga yatokanayo na uharibifu wa mazingira.
Ametoa wito kwa kila kaya kupanda miti walau mitatu, ikiwa ni pamoja na miti ya kivuli pamoja na matunda. Amesema upandaji wa miti utasaidia kuhifadhi miundombinu ya barabara na madaraja.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Bw. Remidius Emmanuel amesema Wilaya ya yake inaendelea kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kutunza mazingira ikiwemo kutokata miti, kutoharibu vyanzo vya maji, kutovamia misitu, kupanda miti na kuhifadhi visiki asili na takribani visiki hai 1,470,252 vimeainishwa na kutunzwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...