Na Said Mwishehe,Michuzi TV

BALOZI mpya wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui ameshiriki mjadala uliopewa jina la Startups ambao umewakutanisha wadau mbalimbali kujadili hatua zinazoweza kuchukuliwa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa wanaoanzisha kampuni na shughuli za ujasiriamali.

Mjadala huo umefanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Alliance Francaise kilichopo jijini Dar es Salaam ambacho kipo chini ya Ubalozi huo ambapo pamoja na mambo mengine Balozi Hajlaoui ametoa pongezi kwa Serikali ya Tanzania kwa hatua inazochukua kwa kuwa mstari wa mbele kukabiliana na changamoto za mabadiliko ta tabianchi.

Balozi huyo mbali ya kutoa pongezi kwa hatua zinazochukuliwa na Serikali kukabiliana na changamoyo hizo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baaada ya kutoa hotuba yake ya kwanza aliyoitoa katika Mkutano wa 76 wa Umoja wa Mataifa nchini Marekani katika kuunga mkono mabadiliko ya tabianchi duniani.

"Nimeisikia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasssan aliyoitoa kwenye Mkutano wa UN kuhusu hatua ambazo Serikali yake inachukua katika kupambana na changamoto za mabadiliko hayo, huku akiweka wazi umefika wakati wa kuhakikisha dunia inaendelea kuwa sehemu salama ya kuishi licha ya changamoto hizo,"amesema na kufafanua Startups ni ni muhimu katika nyanja mbalimbali pamoja na kuweka usawa wa kijinsia katika shughuli za kiuchumi.

Wakati kuhusu majadiliano yaliyofanyika kwenye kituo hicho cha utamaduni, amefafanu anayo furaha kuona vijana wa kitanzania wakikutana na kuweka mikakati ya pamoja katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Katika mdahalo huo ambao umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wamefafanua kwa kina hatua ambazo wanaona zinastahili kuchukuliwa katika kuwawezesha wanaonza shughuli mbalimbali za kiuchumi kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza kwenye majadiliano hayo Mkurugenzi wa Ushirika wa Wajasiriamali Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SuGEco) Revocatus Kimario ameeleza namna vijana wanavyojihusisha na kuwainua vijana ambao wamejikita kwenye shughuli za kilimo katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

"Moja ya kazi zetu kubwa ni kufanya kazi na vijana ili waweze kuwekeza kwenye kilimo kwa lengo la kujiajiri lakini pia kutengeneza fursa kwa wengine, vijana hawa wengi ndio wanaanza biashara , kwa hiyo ni Startups na tukiwangaalia sturtups kwa maana ya wanaoingia kwenye mfumo wa kilimo mabadiliko ya tabianchi yanaaathiri .

"Lakini hata unapojishughulisha na kilimo na chenyewe kinachangia kuleta mabadiliko kwenye mabadiliko ya tabianchi, kwa hiyo pande zote mbili zinapata madhara, sasa hivi tunasema ili uwekeze kwenye kilimo chenye tija ni lazima uwe na uhakika wa uzalishaji, hivyo suala la umwagiliaji ni la umuhimu.

"Kwa mfano mwaka huu Mamlaka ya Hali ya Hewa watametangaza kuna uhaba wa mvua , ukiangalia wiki hii pia Mamlaka ya Bonde la Mto Ruvu na Wami wamekataza matumizi ya ziada ya maji ya ule mto, maana yake wanaoathirika ni Startups walioko kwenye kilimo...

"Maana yake hawawezi kumwagilia, kama walikopa fedha benki na anataka kufanya kilimo cha umwagiliaji tayari kuna mambo yametokea na yametokea kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi,"amesema Kimari.

Amesema kutoka na hali hiyo lazima wadau wawe na mbadala ambao ni teknolojia ambao utasaidia kukabiliana na changamoto zilizopo.


Wakati huo huo Jumanne Mtambalike ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Sahara Ventures amesema wanajihusisha na masuala ya ubunifu , ujasiriamali na teknolojia ambapo wanao vijana ambao wanawasaidia kupata mikopo kama mitaji ya kuendesha biashara zao , pia wanawasaidia kuelewa fursa mbalimbali katika ukuzaji wa biashara zao.


"Leo tuko hapa mimi pamoja na wazungumzaji wenzangu , mjadala mkubwa ni kuhusiana na Startups au kampuni ambazo zinakuwa kwa kasi na mabadiliko ya tabianchi , tunabadilishana mawazo , changamoto na fursa zilizopo kwa ajili ya kampuni hizo na namna gani mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusaidia kwenye ukuaji wa biashara zao kwa kupata wawekezaji lakini na wadau wengine wa kushirikiana nao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Alliance Francaise Flora Valleur ametumia nafasi hiyo kuelezea ratiba ya matamasha yanayoandaliwa na kituo hicho katika kukuza utamaduni na kuboresha ushirikiano wa Ufaransa na nchi nyingine ikiwemo ya Tanzania.

"Wakati wa Covid-19 kituo hiki kilisitisha shughuli za utamaduni kidogo lakini sasa tumeanza tena shughuli za sanaa na utamaduni na tumefanya kazi nzuri na kwa bidiii na tunaendelea,kuanzia Oktoba 6 mwaka huu kila Jumatano tutakuwa na muziki , itakayokuwa inaanza saa moja jioni na tutakuwa na wanamuziki mbalimbali kutoka Afrika Mashariki,"amesema. 

Wadau wakiendelea na majadiliano katika mjadala uliolenga kuangalia mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi hasa kwa Watanzania wanaoanzisha kampuni mpya.Mjadala huo ulipewa jinaa Startups ambapo Balozi mpya wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui alishiriki na kutoa hotuba yake kwa wageni waalikwa.

Balozi mpya wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui(kulia) akijadiliana jambo na mkewe( wa pili kulia) kabla ya kwenda kutoa hotuba yake kwa wadau mbalimbali waliohudhuria Mjadala wa Startups uliofanyika katika Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Ufaransa , Allliance Francaise

Baadhi ya washiriki wa mdahalo wakiwa kwenye viti wakimsubiri Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui ambaye alikuwa mgeni rasmi katika majadiliano ya Startups kwa lengo la kujadili hatua za kuchukua katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi hasa kwa watu ambao ndio wanaanza kujihusisha na shughuli za ujasiriamali nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...