Na Linda Shebby ,Rufiji Mkoani Pwani
BENKI ya NMB imekabidhi viti na meza 50 vyenye thamani ya Shilingi Mil4.5 kwa Shule ya Sekondari Utete iliyopo Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani.
Akikabidhi samani hizo Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki Harold Haule Lambilaki alisema kuwa meza na viti hivyo vilivyotolewa vimetokana na faida ambayo Benki ya NMB wanazipata ambapo wamejikita kurejesha kwa jamii katika miradi ya elimu, afya, ambapo pia hutoa vitanda na magodoro hasa katika hospital za vijijini na mjanga yanayotokea kwa dharura.
"Hadi hivi Sasa tayari NMB tumesha toa misaada yenye thamani ya Bili.8" alisema Kaimu Meneja Kanda ya Mashariki Lambileki
Akizungumza Mara baada ya kupokea samani hizo Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowelo aliwashukuru NMB kwa kutoa viti na meza kwa Shule hiyo ya utete huku akiwasisitiza wanafunzi pamoja na uongozi wa Shule hiyo kutunza ipasavyo samani hizo Ili ziweze kuwafaa wanafunzi wengine watakao kuja kusoma baada yao.
Naye Kaimu Afisa Elimu Wizara ya Msingi Mwalimu Fatuma Kimolo alitoa Shukran kwa NMB kwa kutoa msaada huo.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Utete Bassa Hilary Ngela alisema kuwa shule hiyo ilianzishwa mwaka 1940 ambapo ilikua Shule ya Msingi na baadaye ikapandishwa daraja kuwa shule ya Sekondari mwaka 1990 kwa sasa inawanafunzi 1361 ambapo wavulana 837 na wasichana 524 huku akibainisha kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa majengo, bwalo la kulia chakula kwa wanafunzi na upungufu wa vitanda vya kulalia wanafunzi hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kutatua changamoto hizo.
Mwalimu Ngella alisema kuwa anatoa shukran kwani msaada huo itasaidia kupunguza uhaba viti na madawati shule ni hapo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...