Na Jamaly Mussa, DSJ.
BONDIA maarufu anayeyokea Jamhuri ya Uphilipino Emmanuel Dapidran Pacquiao a.k.a Manny Pacquiao ametangaza kuwania Urais wa wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2022.
Manny Pacquiao aliamua kujipumzisha kwenye masumbwi na kuamua kujikita kwenye siasa tokea mwaka 2010 baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge na baadae kuteuliwa kuwa Seneta, ametarajiwa kwa muda mrefu kutangaza nia yake ya kugombea Urais wa nchi hiyo ya Uphilipino na nia hiyo kaitolea tamko rasmi leo hii.
Bondia na mwanasiasa huyo ameamua kugombea Urais kupitia chama cha Patrido Demokratiko Pilipino (PDP) na amefikia uamuzi huo baada ya kujihusisha na masuala ya siasa kwa muda mrefu, hivyo kwa miaka tisa amekuwa akijihusisha na siasa.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagramu leo Septemba 20,2021 bondia huyo amethibitisha na kutangaza rasmi nia yake ya kugombea Urais. "Leo nakubari kwa ujasiri kuwania Urais wa Jamuhuri ya Uphilipino, na ujumbe kwa wale ambao watafaidika na watu wa Uphilipino; wakati wao umekwisha mimi mpambanaji Manny Pacquia."
Hivyo, kilichochosababisha kuwania nafasi hiyo kubwa ni kutokana na umakini wake mkubwa katika masuala ya siasa pia kuaminiwa na watu wa Uphilipino tokea siku ya kwanza alipo chaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010 ndio imani hio inayomfanya apate ujasiri wa kugombea Urais.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...