Na Amiri Kilagalila,Njombe
Katibu mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo amesema ni lazima kiwanda cha dawa muhimu za binadamu kinachojengwa na MSD huko Idofi halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe kikamilike na hakuna atakayekwamisha jitihada za ujenzi huo kama inavyoelezwa.
Chongolo ametoa kauli hiyo alipozulu mkoani Njombe na kufika kiwandani hapo ambapo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Jasely Mwamwala amesema kumetokea baadhi ya washindani kuanza kuweka vikwazo vya ujenzi wa kiwanda hicho kauli iliyoungwa mkono na mbunge wa Makambako Deo Sanga.
“Sisi wananjombe kiwanda hiki kimejengwa kwetu na kitatusaidia sana kutuongezea hali ya afya kuwa nzuri kwasababu tumejhenga hospitali nyingi na vituo vya afya lakini dawa hakuna.Mh, kiwanda hiki kinapigwa vita sana na wazalishaji wengine kwasababu wanajua watakosa biashara”alisema Mwamwala
Kauli hiyo imemuinua katibu mkuu CCM taifa Daniel Chongolo na kuwahakikishia kiwanda hicho kukamilika na kitaanza kutengeneza dawa hizo.
“Hapa iwe jua iwe mvua,huu mradi utafika mwisho na zikitakiwa fedha za ziada zitakuja kwa umoja wetu huu tulichokiona tunaomba kiendelee na kwenye serikali hii anayefuata ni katibu wengine wote ni wajumbe kwenye vikao vyetu,na sisi wala hatutapiga kelele tunajua pa kupitia”alisema Chongolo
Awali waziri wa afya Dkt Dorothy Gwajima amesema changamoto ya upungufu wa dawa itakwenda kukoma kabisa endapo kiwanda hicho kikikamilika pamoja na viwanda vingine kikiwemo cha keko jijini Dar es Salaam.
“Lakini kwasababu ya maono ya Chama cha Mapinduzi na msukumo wa Rais wetu akasema hapana twendeni kwenye kiwanda ninawapa pesa,na Gloves zitakazozalishwa hapa zitakuwa pair milioni 104 na sisi uzalishaji wetu hapa Tanzania ulikuwa chini ya 20%
Ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu huko Idofi Makambako ungali unaendelea chini ya bohari ya dawa MSD kupitia wizara ya afya ikiwa kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 18 zimewekezwa katika ujenzi huo.
Katibu mkuu wa CCM taifa Daniel Chongolo akieleza namna watakavoshirikiana ili kukamilisha ujenzi wa kiwanda hicho kilichopo mkoani Njombe.
Waziri wa afya Dkt Dorothy Gwajima akiwaeleza mamia ya wananchi faida ya kiwanda cha dawa kinachojengwa mkoani Njombe mara baada ya kukamilika kwake na umuhimu wake kwa taifa.
Miongoni mwa vifaa vinavyoendelea kufungwa katika kiwanda cha dawa mjini Makambako
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...