Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akifungua Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Kongamano hilo limefanyika hii leo 23/09/2021 katika Ukumbi wa Royal Village Dodoma. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba, Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari.
Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akihutubia wadau walioshiriki kongamano la Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. Mhe. Balozi amesisitiza kuendelea kushirikiana na Tanzania katika jitihada za kukabiliana na athari za Mabadiliko ya Tabianchi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akiteta jambo na Mkurugenzi wa REPOA Dkt. Donald Mmari (kushoto) mara baada ya kufungua Kongamano la Wadau wa Kitaifa kuhusu upatikanaji wa Rasilimali za kusaidia utekelezaji wa Mikakati ya Taifa ya Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi  hii leo katika ukumbi wa Royal Village Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Dkt. Andrew Komba.
Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar akizungumza na Bw. Richard Muyungi ambaye ni Mjumbe wa Green Climate Fund kwa niaba ya Afrika, kuhusu Maandalizi ya Mkutano wa Glasgow hasa matarajio ya Afrika na Tanzania katika Mkutano huo kuhusu upatikanaji wa fedha za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...