Baadhi ya Wanamuziki kupitia Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) wakiwa na Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam jana  ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Muziki Duniani ambayo kitaifa kwa mara ya kwanza yataadhimishwa  Jijini Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia  Septemba 24 hadi OKtoba 1 ambapo ndio itakuwa kilele chake.
Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakiwa shuleni hapo walipotembelewa na wanamziki hao jana.
Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Jangwani wakiwa katika picha ya pamoja na wanamziki hao
Baadhi ya Wanamuziki kupitia Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) wakipata maelezo walipotembelea Makumbusho ya Taifa ya Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya picha zilizomo Makumbusho ya Taifa ya Jijini Dar es Salaam.


Na Dotto Mwaibale 


WANAMUZIKI mbalimbali kupitia Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) jana Wamefanya ziara ya matendo ya huruma na Kuhamasisha shughuli za maendeleo  ya jamii ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Muziki Duniani ambayo kitaifa kwa mara ya kwanza yataadhimishwa  Jijini Arusha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia  Septemba 24 hadi OKtoba 1 ambapo ndio itakuwa kilele chake.

Akizungumzia ziara hiyo Katibu Mkuu wa TAMUFO Stella Joel alisema katika ziara hiyo wanamuziki hao  walitembelea Shule ya Sekondari ya Jangwani ya  jijini Dar es Slaam ambapo waliweza kujumuika na kutoa zawadi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum na baada ya hapo waliendelea na ziara hiyo ya uhamasishaji wa maendeleo kwenda maeneo mengine yakiwemo Makumbusho ya Taifa ya Jijini Dar es Salaam.

Joel alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi na wanamuziki wote kushiriki maadhimisho hayo kwa kujitokeza kwa wingi siku hizo za maadhimisho hayo kuelekea Oktoba 1, 2021 ambayo itakuwa ni kilele chake ambapo kutakuwa na mambo mengi na burudani kubwa ya muziki kutoka  kada tofauti ya wanamuziki wakiwepo wa Bongo Fleva, Dansi, Zuku, Injili, ngoma za asili na mingine mingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...