Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam ,Omary Kumbilamoto leo amekagua barabara ya Mtaa wa kwa Kombo kata ya Vingunguti ambayo anaikarabati kwa kiwango cha zege.
Kumbilamoto ambae aliamua kujenga barabara hiyo mara baada ya kubaini Kero zinazowapata wakazi wa eneo hilo na Mitaa ya jirani.
Amesema kuwa mara baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi wa eneo hilo aliamua kumwita mhandisi wa Manispaa na kufanya tathmini ndogo kuhusu eneo hilo na kufikia Muafaka kuwa pajengwe kipande cha zege .
"Eneo hili lilikuwa korofi na halipitiki si kwa pikipiki ama gari, hasa wakati wa mvua na ukizingatia ndio njia kubwa inayounganisha Wakazi wa kombo na Tabata, hivyo mara baada ya kukamilika hapa sasa watu watapata urahisi wa kusafirisha mizigo yao na wao kusafiri bila hofu" Amesema Kumbilamoto.
Ametaja kuwa Moja ya matatizo makubwa ya barabara hiyo ilikuwa inatishia nyumba za watu kuanguka na kusababisha ajali kwa Vijana wa bodaboda pindi wanapopakia abiria.
Ametaja kuwa wao Kama Viongozi wamepokea maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kutatua Kero za watu hivyo ndio maana ameamua kujenga kipande hicho kwa fedha zake mfukoni.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto akimsikiliza mmoja wa Wakazi wa jirani na barabara hiyo kuhudu adha waliyokuwa wanapata kabla ya barabara kujengwa
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto akizungumza na Wazee wa mtaa wa kwa Kombo
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omar Kumbilamoto akizungumza na Vijana wa Vingunguti mara baada ya kutoka kukagua barabara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...