Na Jamaly Mussa, DSJ
MWANADADA Staa katika tasnia ya filamu nchini Elizabeth Michael maarufu Lulu amesema katika maisha hakuwahi kufikiria kama atakuja kuolewa na mwanaume ambaye ameshapata watoto na mwanamke mwingine.
Lulu amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagramu baada ya kuamua kuwajibu baadhi ya mashabiki zake waliokuwa wanataka kujua anawezaje kulea watoto wawili ambapo mmoja ni wake aliyezaa na mumewe Majizo na mwingine wa Hamisa Mobeto.
Kabla ya Lulu kuolewa na Majizo, tayari Majizo alishapata mtoto na Hamisa Mobeto , hivyo kwa sasa analea watoto wote wawili."Sikutamani kabisa kuzaa na mwanaume ambaye tayari ana mtoto ,nilikuwa na ndoto ya kuolewa na mwanaume tutakayeanzisha familia pamoja, sio kuwa na mume mwenye mtoto nje ya ndoa kama dini inavyosema."
Akiendelea kuwajibu mashabiki zake Lulu amesema alikuja kugundua kuwa binadamu hajakamilika wakati mwingine sio hadi awe kilema ndio aonekane haujakamilika."Kuna mambo mengine yanaweza kusimama kama kilema."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...