Na Kassim Nyaki-NCAA

Makamanda na maafisa 110 kutoka wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu-Duluti kilichopo Mkoani Arusha wametembelea Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali za Uhifadhi, utalii na mazingira katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.

 

Ujumbe wa makamanda na maafisa hao ulioongozwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu-Duluti Brigedia Jenarali Sylvest Damian Ghuliku unajumuisha Maafisa kutoka Nchi za Rwanda, Burundi, Kenya, Malawi, Eswatini, Msumbiji, Nigeria, Bangladesh, Misri, Uganda na wenyeji Tanzania.

 

Brigedia Jenerali Ghuliku amebainisha kuwa pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani kwa maafisa hao wa jeshi,  Chuo hicho kinachojumuisha maafisa kutoka Nchi mbalimbali wanaokuja Tanzania  kinatumia ziara hiyo kama fursa ya kutangaza  uzuri na vivutio vya kipekee vilivyoko Tanzania.

 

“Sisi kama wazalendo tunapaswa kujivunia rasilimali za uhifadhi na utalii tulizonazo. Chuo chetu kinajumuisha maafisa kutoka Nchi mbalimbali tunaamini kupitia ziara hii watakuwa wamejifunza mambo mengi na watakuwa mabalozi wazuri wa kutangaza vivutio vyetu watakaporudi kwenye Nchi zao baada ya program ya masomo yao kukamilika hapa Nchini” alifafanua Brigedia Jenerali Ghuliku.

 

Naibu Kamishna wa NCAA (Uhifadhi, Utalii na Maendeleo ya Jamii), Dkt. Christopher Timbuka ameshukuru ujumbe wa Maafisa wa jeshi kwa uamuzi wa kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na kuwahakikishia kuwa NCAA itaendelea kushirikiana na Chuo hicho katika programu za kutoa uelewa wa shughuli za uhifadhi, Utalii na maendeleo ya Jamii. 

 

Kabla ya kutembelea vivutio vilivyoko ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ujumbe huo ulipokea mada kuhusu historia ya eneo la Ngorongoro, shughuli za utalii, uhifadhi na maendeleo ya Jamii.

Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu-Duluti, Brigedia Jenerali Sylivest Damiam Ghuliku (katikati) akipewa ufafanuzi kushusu shughuli za Uhifadhi na Utili kutoka wa Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA Dkt. Christopher Timbuka (kulia)


Naibu Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dkt. Christoher Timbuka (wa tatu kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Chuo cha Ukomando na Unadhimu-Duluti Mkoani Arusha waliofika Ngorongoro kwa ya ziara ya mafunzo na kutembelea vivutio vya utalii katika Hifadhi hiyo.


Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa NCAA (Huduma za Ulinzi) Elibariki Bajuta akitoa mada kuhusu Historia ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa Maafisa wa Chuo cha Ukamanda na Unadhibu-Duluti (hawapo pichani) wakati ya ziara ya mafunzo na utalii katika Hifadhi ya Ngorongoro.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...