Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
KAMPUNI ya usambazaji na uuzaji wa gesi ya Oryx nchini Tanzania imesaini mkataba wa hali bora za wafanyakazi, ambapo katika mkataba huo yapo makubaliano ya kuwasomesha watoto wao kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita.
Pia kuna kipengele kinachotoa nafasi ya saa mbili kwa mama mwenye mtoto mchanga kwenda kunyonyesha hadi hapo atakapofikisha miezi sita.Utiaji wa saini wa makubaliano hayo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama na Dk Aggrey Mlimuka ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) walishuhudia walishuhudia utiwaji saini huo uliofanywa kati ya Katibu Mkuu wa TUICO Boniphace Nkakatisi na Mkurugenzi wa kampuni ya mafuta, Kalpesh Mehta.
Baada ya kusainiwa mkataba huo huo, Waziri Mhagama amesema amefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na kampuni hiyo kwani inarahishia Serikali kutekeleza sheria za kazi huku akisisitiza kuwa utawasukuma wafanyakazi kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuleta tija kwa kampuni.
Waziri Mhagama amewashauri wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na wala hakuna sababu ya kubweteka ili watakaposaini mkataba mwingine hapo baadaye mambo mazuri yaendelee kuongezeka.
"Pia Latina mkataba huu nimefurahishwa kutengwa muda wa mama kunyonyesha, nishauri kama inawezekana kampuni siku za usoni itenge na chumba maalum kwa ajili ya wakina mama wanaotaka kunyonyeshea watoto wao ofisini hadi hapo watakapokoma kunyonya,"amesema.
Awali Mwenyekiti TUICO, Boniface Mkakatisi, ametoa shukrani kwa majadiliano kati ya wafanyakazi na kampuni kwenda vizuri hadi kifikia hapo jambo ambalo ni nadra kwa kampuni zingine ambazo hata uongozi na wafanyakazi kukaa meza moja ni shida.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Dk Aggrey Mlimuka, amefafanua mkataba huo kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake ili pande zote mbili ziweze kufaidika nao.
"Kampuni zingine zinaweza kuiga haya kama watakubali kuwa na njia za majadiliano ambazo zitasaidia pia kampuni zao kusonga mbele kwa kuwa wafanyakazi sasa watafanya kazi wakiwa na uhakika na maisha yao,"amesisitiza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa hafla ya uwekaji saini mkataba wa hiari wa Hali bora baina ya Menejimenti ya Makampuni ya ORYX energies na Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani, biashara, Taasisi za fedha, huduma na ushauri (TUICO) jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka akizungumza wakati wa hafla uwekaji saini mkataba wa hiyari wa Hali bora baina ya Menejimenti ya Makampuni ya ORYX Energies na Chama cha Wafanyakazi wa Viwandani, biashara, Taasisi za fedha, huduma na ushauri (TUICO).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt. Aggrey Mlimuka (kulia kwake), wakione hati za makubaliano hayo mara baada ya zoezi la uwekeji saini kukamilika wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu wa TUICO, Boniphace Nkakatisi na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya mafuta, Kalpesh Mehta na Mkurugenzi wa makampuni ya ORYX Tanzania Bw. Benoit Aramari (wa pili kutoka kushoto).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katika) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya ORYX mara baada zoezi la kusaini hati za makubaliano kati yao na TUICO.( Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...