Na Sixmund J. Begashe.
Makumbusho
ya Taifa la Tanzania imepokea ugeni wa Uongozi na Wataalam wa
Makumbusho ya Taifa ya nchi ya Malawi ambao utakuwa nchini kwa siku sita
ili kupata uzoefu wa namna ya uendeshaji wa shughuli za kimakumbusho.
Akiwapokea
wageni hao katika uwanja wa ndege wa Mwl Nyeyere Dar es Salaam, Mratibu
wa program ya wageni hao wa Makumbusho ya Taifa nchini, Bi Frida Kombe
amesema ni faraja kubwa kuona nchi za nje zinaiona Tanzania kama Mwalimu
wa uhifadhi wa Urithi wa Utamaduni na Malikale.
Wakiwa
nchini, licha ya kujifunza shughuli za uhifadhi pia siku ya Ijumaa
tarehe 24 September 2021 watapata nafasi ya kutanzama maonesho ya Museum
Art Explosion, kufanya Utalii katika jiji la Dar es Salaam (Dar City
Tour) na Bagamoyo Mkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...