Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MBUNGE
wa Vijana Taifa kupitia Mkoa wa Manyara, Asia Halamga ameongoza
harambee ya kukusanya fedha za ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM
Wilayani Simanjiro na kufanikisha kupatikana kwa shilingi milioni 6.9
Asia
ameongoza harambee hiyo iliyofanyika jana mji mdogo wa Mirerani kwenye
kikao cha baraza la UVCCM Wilayani Simanjiro, ambapo fedha taslimu
zilipatikana shilingi milioni 2.8 na ahadi shilingi milioni 4.1
Hata
hivyo, Mbunge huyo Asia amewaahidi vijana hao kuwa atafanikisha gharama
ya kufunga nyaya za umeme pindi nyumba hiyo ya katibu wa UVCCM wilaya
ya Simanjiro ikifikia hatua hiyo.
“Huu
siyo mwisho wa kushirikiana nanyi kwani Simanjiro mmekuwa bega kwa bega
nami hivyo tutaendelea kuungana mkono kwenye maendeleo bila wasiwasi
wowote ule, amesema Asia.
Mbunge
wa jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka amempongeza Asia kwa
namna anavyomuunga mkono Bungenni kutetea maslahi ya wana Simanjiro.
“Tunapaswa
kumkumbuka Asia kwa moyo wake wa upendo kwani alilia nasi Bungeni
kipindi cha wadau wa madini wapekuliwa bila staha, waswahili wanasema
mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,” amesema Ole Sendeka.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Baraka Kanunga amewapongeza
viongozi wa UVCCM wa wilaya hiyo kwa dhamira ya ujenzi wa jengo hilo.
Mwenyekiti
wa UVCCM Wilaya ya Simanjiro, Thomas Mollel amemshukuru Mbunge huyo
Asia kwa kufanikisha harambee hiyo ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wao
wa wilaya yao.
Katibu wa
UVCCM Wilaya ya Simanjiro, Bakari Mwacha amesema ujenzi wa nyumba hiyo
utaendelea wiki ijayo kwani harambee hiyo imefanikisha fedha
zitakazonunua vifaa.
Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, Kiria Laizer amesema
anachangia shilingi milioni 2 kwani jumuiya hiyo imemlea akiwa
Mwenyekiti wa Wilaya hiyo kwa miaka miwili na alishachangia ujenzi wa
ofisi pia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...