Mdau wa Maendeleo wa wilaya ya Hanang mkoani Manyara Clentine Fissoo ameahidi kutoa mifuko 200 ya saruji kwa shule ya msingi Bassotughang kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo.
Akizungumza kwenye mahafali ya 22 katika shule hiyo mdau huyo amesema ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa na changamoto ya miundombinu ya shule hiyo.
Fissoo ameueleza uongozi wa shule ya msingi kuwasiliana nae muda wowote ili kupatiwa mifuko hiyo ya Saruji.
Hata hivyo amesema kuwepo kwa miundombinu rafiki katika shule hiyo kutaongeza ari ya wanafunzi kusoma na kuongeza ufaulu.
Risala iliyoandaliwa na mkuu wa shule hiyo Mwalimu Antony Marwa imeeleza kuwa shule hiyo ina wanafunzi 589 wakiwemo wavulana 237 na wasichana 352 wakianzia darasa la awali hadi la saba.
Sehemu ya risala hiyo imeendelea kueleza kuwa shule ina upungufu wa miundombinu mbalimbali ambapo ina nyumba nne za walimu kati ya tisa zinavyohitajika, madarasa kumi kati ya 14 yanayopaswa kuwepo,matundu nane ya vyoo vya wanafunzi kati ya 22 yanayohitajika huku nane yaliyopo yakikosa sifa kwa kuwa haajakidhi vigezo husika kwani havina milango na kimo cha paa ni kifupi.
Changamoto nyingine inayoikabili shule hiyo ni ukosefu wa kabati la kuhifadhia vitabu hivyo vitabu kusalia kwenye maboksi na kupelekea kuharibiwa na mchwa na panya. Jumla ya wanafunzi 54 sawa na asilimia 71 wamehitimu elimu yao ya msingi katika shule ya Bassotughang huku 22 asilimia 29 wakishindwa kumaliza darasa la saba kutokana na sababu mbalimbali.
Na John Walter-Manyara
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...