Na YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO.

Mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Jairy Khanga alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwawewzesha wataalamu wa afya kwenda kutoa huduma za chanjo kwa wananchi kwa kutoa elimu ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kuchanja.

Dkt Khanga amedai mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa afya hao watawezeshwa njia na mbinu za kuelimisha jamii pamoja na kupambana na changamoto zitakazopatikana kutoka kwa wananchi aweze kutoa elimu ya kuwaelimisha wananchi na waweze kuchanjwa.

‘’Wananchi hawana taarifa sahihi kuhusu chanjo ndio maana mwamko wa wananchi katika swala la kuchanja ni dogo hivyo tunatakiwa kuimarisha dhana ya mawasiliano na kuwafanya wananchi wengi waweze kupata tarifa sahihi na kubadilisha fikra potofu walizonazo  na wakubali kuchanja alisema” Dkt Khanga

Hata hivyo aliwataka  watoa huduma za chanjo katika mkoa wa Ruvuma kushiriki mafunzo ya siku mbili ya kujengewa uwezo katika utoaji chanjo katika Halmashauri za wilaya zote za mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwafanya wananchi wahamasike katika zoezi la kuchanja.

Aidha pamoja na mambo mengine alimpongeza afisa afya mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru  bwana Arnold Herman na mratibu wa elimu ya afya kwa jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Ally Yassin Ndambile kwa kuhamasisha jamii kuhusu kupata chanjo.

William Reuben kiongozi wa timu ya kitaifa ya chanjo katika mkoa wa Ruvuma amewataka washiriki wa mafunzo kuleta matokeo katika kazi watakazotakiwa kwenda kuzifanya ili kutekeleza lengo la saerikali la kuhakikisha wananchi wake wanapata chanjo .

Mada zinazofundishwa katika mafunzo hayo ni mada 8 ambapo kwa siku ya kwanza mada ya sayansi ya jamii,mawasiliano juu ya chanjo ,mabadiliko ya tabia , utaratibu na usimamizi shirikishi kwa jamii na mada zingine 4 zitafundishwa siku ya pili. 


 

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...