Mkurugenzi wa Mtendaji ANGOZA hassan Khamis Juma (katikati)akifafanua jambo wakati akitoa hotuba kwa Waandishi wa Wabari kuhusiana na Mkutano utakao fanyika katika Ukumbi wa Madinatul-bahari utakao zungumzia kuhusu Kukuza Ubia na Majadiliano kuhusiana na mikakati ya Kitaifa ,Kikanda na Kimataifa uliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.wa mwanzo kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Kitaifa Tume ya Mipango Jamila Abdalla Seif na kushoto ni Mwakilishi kutoka shirika la Umoja wa mataifa la mipango ya maendeleo (UNDP)Kimwaga Muhiddin Ali.
Na Rahma Khamis Maelezo 21/9/2021
MKUTANO wa kukuza Ubia na Majadaliano na Utekelezaji wa Mikakati ya kitaifa,kikanda na kimataifa kati ya wadau wa taasisi binafsi na watendaji wa Serikali visiwani Zanzibar unatarajiwa kufanyika kesho Madinatu Albahar Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji kutoka Tume ya Mipango Zanzibar Hassan Yussuf Juma katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo amesema mkutano huo utawashirikisha zaidi ya washiriki 100 kutoka Unguja na Pemba.
Alisema katika mkutano huo wanatarajia kujadili malengo mbalimbali ya kimsingi ambayo yatakuza sekta zote kiuchumi ikiwemo kujadili na kutengeza mikakati ambayo itahakikisha majukumu ya Serikali na wadau wengine katika kutekeleza na kufikia shabaha ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030.
Malengo mengine ni kukuza ubia uliopo baina ya Serikali na sekta binafsi pamoja asasi za kirai katika utekelezaji wa malengoya maendeleo endelevu Zanzibar.na kupata mapendekezo na shughuli ambazo zitachukuliwa na kufanyiwa kazi na UNDP,ZPC,Sekta binfsi Asasi za kiraia na wadau muhimu wa utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Zanzibar.
Aidha amesema kuwa katika mkutano huo mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo mchango wa Asasi za Kiraia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu Zanzibar , Ushiriki wa Sekta binafsi na matokeo ya maendeleo endelevu Zanzibar pamoja na Mchanganuo wa Taarifa kijinsia katika ufatiliaji na kuripoti malengo ya maendeleo endelevu Zanzbar.
“Mada ya mwisho itahusiana na Uratibu, Utekelezaji, Ufatiliaji Tathmini ya Mipang ya Maendeleo Endelevu ya Kitaifa,Kikanda na Kimataifa, ambapo washiriki wa Kongamano hilo watapata fursa ya kuchangia mada zote hizo,”alisema Mkurugenzi huyo.
Nae Mkuu wa kitengo cha Ufatiliaji na Tathmini Tume ya Mipango Jamila Abdallah Seif amesema watu wengi wamekua na uelewa mkubwa na agenda 2030 ambayo utekelezaji wake ulianza Zanzibar tokea mwaka 2019 na kufanyika mikutano katika ngazi ya jamii na waandishi wa habari waliokuwa wakitoa ripoti kwa kila mkutano uliofanyika katika sehemu husika.
Aidha amefahamisha kuwa mkutano huo ulijikita katika kuzungumza juu ya malengo ya maendeleo endelevu Mjini na Vijijini hivyo wanawashukuru kwa kuwasaidia kukuza uwelewa wa wananchi.
Mkutano huo unaoandaliwa na kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango,Sekta Binafsi na Asasi za Kiraia ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kua Waziri a nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Mh Jamal Kassim Ali na Kaulimbiu ya mwaka huu KUKUZA UBIA WA SERIKALI KITAIFA KIKANDA NA KIMATAIFA KUTAPELEKA KUFIKIA MALENGO YALIYOKUSUDIWAKWA HARAKA ZAIDI.
Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini Kitaifa Tume ya Mipango Jamila Abdalla Seif akitoa ufafanuzi baadhi ya maswali yalioulizwa katika mkutano wa Waandishi wa Habari ulioandaliwa kwa pamoja kati ya Tume ya Mipango Sekta binafsi na Asasi za Kiraia kuhusiana na kukuza Ubia na Majadiliano kuhusu mikakati ya kitaifa Kikanda na Kimataifa uliofanyika katika Ukumbi wa sanaa Rahaleo Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...