Na Hamida Kamchalla, KILINDI.
Mlezi
wa Chama cha Mapinduzi (Ccm) Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Makamu wa pili
wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hemedi Suleiman Abdallah
amewahimiza wananchi kuachana na maneno yanayopotosha badala yake
kujitokeza kwa wingi kwenda kupata chanjo ya Uviko 19 ili kuendelea kuwa
salama ikiwa ni pamoja na kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na
makazi pindi itakapoanza.
Makamu
huyo aliyasema hayo jana (leo) wakati akizungumza na wananchi wa kata
ya Kibirashi wilayani Kilindi alipofanya ziara ya kikazi na pia kuzindua
mashina ya chama hicho.
"Wananchi
wenzangu, tunafahamu kama kuna huu ugonjwa wa Uviko 19, na serikali
imechukua juhudi kubwa ya kuleta chanjo, wapo watu ambao wanababaisha,
wanajaribu kutoa lugha tofauti kuwapotpsha watu, ndugu zangu wa
Kibirashi na maeneo mengi ya jirani, chanjo zipo nadhani utaratibu
kwenye Mkoa upo, twendeni tukapige chanjo tujikinge, chanjo ni bora
kuliko kutibu" alisisitiza.
"Jingine
ni kuhusu suala la sensa, Rais wa Jamuhuri ya Muungano ameshazindua
zoezi la sensa, madhumuni ya sensa hii ni kuhesabiwa na tujulikane
hesabu yetu ili serikali iweze kupanga mahesabu yake, kwahiyo niwaombe
Wanakilindi na Watanzania wote, wa vyama vyote nimiombeni mjitokeze kwa
wingi tukahesabiwe muda utakapowadia" alisema.
Aidha
Makamu huyo alitoa ahadi ya kushirikiana na viongozi mkoani humo
kuhakikisha wanaifanyia matengenezo barabara itokayo Handeni hadi Songe
huku akisisitiza kwamba barabara hiyo ni muhimu na ina manufaa makubwa
katika kukuza uchumi wa Mkoa kutokana na mradi mkubwa wa ujenzi wa
Bandari.
"Tulipokuja
tumetembea kwenye barabara ya lami, lakini tulipofika Handeni tumeingia
kwenye barabara hii ambayo mmeizungumza, nimepata maelezo yake, na
nimeona umuhimu wa barabara hii, naomba niwahakikishie kwamba sikuja
Wilaya hii wala Mkoa wa Tanga kutembea, nimekuja kuhakikisha ilani ya
Chama cha Mapinduzi inatekelezwa" albainisha.
"Nitashirikiana
na viongozi wenzangu, wapo waheshimiwa wabunge wanafanya kazi nzuri na
mimi nitashirikiana nao, na mimi kwa nafasi yangu kule kwenye kamati
nitapata kuchomekachomeka kwa sababu mwenyekiti anakuwa hayuko mbali"
aliongeza.
Alibainisha
kwamba "faida ya barabara hii ni kubwa sana na siyo kwa Wanakilindi tu
bali ni kwa Watanzania wote, Tanga tuna Bandari, ikitumika vyema Bandari
ya Tanga na barabara hii ikawa rafiki, nakuhakikishieni uchumi wa Mkoa
wetu utakua kwa kiasi kikubwa, kwahiyo nikuhakikishieni suala hili la
barabara tutaenda nalo pamoja".
Hata
hivyo aliwahakikishia wananchi hao kuwatatulia kero nyingine mbalimbali
zilizopo ambazo katika sekta ya maji, elimu pamoja na afya huku akisema
watashirikiana kwa ukaribu katika utekelezaji kwa maslahi ya wananchi
hao.
Awali akizungumza
katika mkutano huo, mbunge wa Kilindi Omari Kigua alielezea kero
zinazoikabili wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za
utekelezaji na hatua zilizofanywa na serikali.
"Katika
sekta ya maji, elimu, afya na umeme, katika shina hili tunayo shule ya
sekondari na hivi leo ninavyozungumza tumeshapewa sh milioni 55 kwa
ajili ya madarasa manne na matundu 12 ya vyoo kwa ajili ya vijana wetu,
lakini pia tumeongezewa sh milioni 48 kwa ajili ya kutatua kero ya maji
katika kata hii ya Kibirashi ambayo shina hili namba tano ipo" alisema.
"Halikadhalika
barabara hii ni ya vumbi muheshimiwa lakini serikali ya Chama cha
Mapinduzi kwa mwaka huu wa fedha imetutengea fedha takribani sh milioni
500 na wana dhamira ya kutengeneza kilomita 20 za barabara kuanzia
Handeni na kwavile wewe ni mlezi utaondoka nalo" aliobngeza.
Mbunge huyo pia alifafanua kwamba
"Kilindi
hii ina madini, mifugo na rasilimali nyingine lakini uchumi wa wananchi
haukui kwasababu ya barabara haipitiki, tunaomba sana, sisi kwetu
tunaona kama leo ni ukombozi, ukitoka hapa utupelekee salamu zetu kwa
mwenyekiti kwamba, mbunge na wananchi wa Ccm wanaomba uwatengenezee
barabara".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...