Na Mwamvua Mwinyi ,Pwani
MKOA
wa Pwani umejipanga kuongeza mapato ya ukusanyaji mapato kupitia vyanzo
vya mapato ya ndani ya halmashauri zake kwa asilimia 100 ili
halmashauri hizo ziweze kujitegemea na kutoa huduma za kimaendeleo kwa
wananchi .
Pia imeelezwa ,uboreshaji wa utoaji huduma za kijamii utasaidia kuondoa migogoro na matatizo kwa wananchi .
Hayo
yalisemwa mjini Kibaha na Katibu Tawala (RAS) mkoa wa Pwani ,Mhandisi
Mwanasha Tumbo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kufungua mafunzo ya utawala bora wa fedha unaosimamiwa na shirika la
maendeleo la ujerumani GIZ pamoja na kufadhiliwa wadau wa maendeleo wa
serikali ya Ujerumani, serikali ya Uswisi kupitia shirika la maendeleo
la Uswisi na umoja wa Ulaya.
Tumbo
alieleza Kwasasa wapo katika asilimia 80,licha ya halmashauri ya
Chalinze kufikia zaidi ya asilimia 100 hivyo watajitahidi halmashauri
nyingine zifikie lengo lao.
Nae
Raymond Nzali ambaye ni mtaalamu mshauri wa mradi wa utawala bora wa
fedha, kutoka GIZ alisema lengo la mafunzo hayo ni kutengeneza mpango
kazi kwa ajili ya ukusanyaji wa mapato .
"Tumelenga
zaidi kwenye ushuru wa huduma ambapo bado uko chini sana licha ya
Halmashauri zilizochaguliwa kuonekana zinafanya vizuri kwenye
ukusanyaji".
Ofisa msimamizi
mkuu wa mradi huo toka TAMISEMI, Ismail Chami alisema, wameuingiza mkoa
wa Pwani kwenye mradi huo kwani nao una vyanzo vingi vya mapato vipya
kupitia viwanda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...