- Akemea Rushwa na Urasimu.

- Asema Serikali ya Mkoa inaunda One stop Center ya Biashara.

- Azielekeza Mamlaka za udhibiti kuweka utaratibu wa kuwatembelea wenye Viwanda kwa pamoja kuepuka usumbufu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewahakikishia Wafanyabiashara na wawekezaji mkoani humo kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira Bora na wezeshi ya biashara kuenda sambamba na azma ya Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuondoa kero za kibiashara.

Akizungumza wakati wa mkutano wa shirikisho la Wenye Viwanda CTI, RC Makalla amesema Serikali ya Mkoa ipo hatua ya mwisho ya kuanzisha One stop Center ya biashara itakayojumuisha Mamlaka zote za udhibiti ikiwemo TBS, NEMC, OSHA, TRA, BRELA, Jeshi la zimamoto, Uhamihaji  ili kupunguza Urasimu.

Aidha RC Makalla ameelekeza Mamlaka zote za udhibiti ikiwemo TBS, NEMC, OSHA, Jeshi la zimamoto, Uhamihaji na nyinginezo kuweka utaratibu wa kutembelea viwanda kwa pamoja ili kuepuka kukinzana kwa matamko ,maelekezo pamoja usumbufu wa kupokea wageni kila siku.

Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza TANROAD na TARURA kurekebisha miundombinu ya Barabara kwenye Maeneo ya Viwanda ili kuondoa kero na changamoto ya uharibifu wa Magari.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...