Na Linda Shebby, Kibaha
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge amesema katika kuhakikisha wanafikia lengo la utoaji wa chanjo ya Uviko 19 , chanjo hiyo itakua ikitolewa nyumba kwa nyumba.
Mkuu huyo wa Mkoa aliyasema hayo leo Kibaha Mkoani Pwani alipokuwa katika ufunguzi wa semina ya Afya ya Msingi ya Mkoa kuhusu chanjo dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 ambapo semina hiyo imewahusisha wakuu wa Wilaya zote kutoka Mkoani Pwani , Kamati ya Ulinzi na Usalama , viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa afya Mkoani hapa
Akizungumzia kuhusu muitikio wa utoaji chanjo hiyo ya Uviko 19 Mkoani Pwani alisema kuwa hadi sasa Mkoa umefikia nusu ya lengo ambapo hali halisi ya waliochanja hadi sasa ni asilimia 50 huku chanjo zilizotolewa 30,000 na achanjo ambazo bado hazijatumika ni 15, 000 kwa Mkoa wa Pwani huku Wilaya mbili za Bagamoyo na Kibaha Mji ndiyo wameongoza kwa muamko wa kupata chanjo hizo.
"Pwani tumejiwekea mpango mkakati wa utoaji chanjo hizi za Uviko 19 ambapo tutawafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ya mikusanyiko,tutapita nyumba kwanyumba ikiwemo kwenye mihadhara ya kidini na makongamano mbalimbali ambapo wengi hupatiwa elimu baada ya kufahamu vizuri faida ya chanjo hizi huridhia kuchanja baada ya kupatiwa taarifa sahihi jinsi chanjo hiyo inavyoweza muhusika aliyechanjwa " alisema Kunenge.
RC Kunenge alisema kuwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ina njema kwa kutoa chanjo hizo kwa wananchi wake huku akisisitiza chanjo ya Uviko 19 liyobaki ikatumike kwa kuwachanja wananchi Ili kuinusuru isiweze kuharibika.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Dokta Gunini Kamba ametoa wito kwa vijana wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 45 kuachana na mawazo potofu kwamba ugonjwa huu hauwadhuru sana vijana kutokana na umri wao mdogo huku akisisitiza kwamba ni muhimu wajitokeze kupata chanjo hiyo itasaidia kuongezea kninga zao za mwili huku akisisitiza kwamba chanjo hizi hazina madhara yeyote kama jinsi inavyo vumishwa na wachache wenye nia ovu.
Dokta Gunini aliongeza kwa kusema kuwa wataahirikiana katika ngazi zote Ili kuhakikisha wanafikia lengo la kutoa chanjo hizo za Uviko 19.
Dokta Gunini aliongeza kwa kusema kuwa utaratibu huu wa kutoa elimu juu ya umuhimu kupata chanjo ya Uviko 19 wameanza nayo tangu walipoanza kutoa chanjo hiyo Mkoani Pwani ambapo wamekua wakitoka elimu kwa wananchi na wadau mbalimbali ikiwemo katika masoko na sehemu mbalimbali zenye mikusanyiko.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...