Mfanyabiashara James Rugemalira akiwa na familia yake nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Septemba 16,2021.

Na Mwandishi wetu
MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP) amefuta mashtaka yanayomkabili Mfanyabiashara James Rugemalira na mahakama kumwachia huru kwa sababu hana nia ya kuendela na mashtaka dhidi yake.

Mapema upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili wa serikali, Grace Mwanga umedai mahakani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi dhidi ya Rugemalira iliitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa lakini DPP amewasilisha hati ya kuiondoa kesi hiyo (Nolle Prosequ) chini ya kifungu cha sheria cha 91 (1) cha mwenendo wa makosa ya jinai.

Licha ya hayo Juni 2017, Taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini Tanzania TAKUKURU iliwafikisha Mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Kufua Umeme (IPTL), Herbinder Seth na Rugemalira kwa makosa sita ya uhujumu uchumi ikiwemo kosa la kuisababishia serikali hasara.Aidha katika shtaka jingine, Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari23,2014 makao makuu ya benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi St Joseph zote za Dar es salaam, kwa ulaghai, walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), USD 22,198,544.60 na shilingi 309, 461,300,158.27. 

Iliendelea kudaiwa kuwa katika shtaka la kusababisha hasara, washtakiwa hao wanadaiwa kwamba mnamo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati Kinondoni kwa vitendo vyao waliisababishia Serikali hasara ya USD 22, 198, 544.60 na Tsh 309,461,300,158.27.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...