Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai (katikati) akiwa na Muanzilishi ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto) wakikata utepe kwenye kitabu kuashiria uzinduzi wa Ajenda ya Mtoto Njiti 2021 uliofanyika leo kwenye hoteli ya Nasheera, jijini Dodoma na kuratibiwa na Taasisi hiyo. Wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, Mbunge wa Maswa, Stanslaus Nyongo na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Maendeleo ya Jamii), Dkt. John Jingu. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Ajenda ya Mtoto Njiti 2021 uliofanyika leo kwenye hoteli ya Nasheera, jijini Dodoma, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel.
Muanzilishi ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njiti nchini, Doris Mollel akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ajenda ya Mtoto Njiti 2021 uliofanyika leo kwenye hoteli ya Nasheera, jijini Dodoma, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...