Na Mwandishi Wetu, Kigoma

KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC) kimeanza mchakato wa kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata mafuta ya mawese ikiwa ni mkakati wa kutatua changamoto ya uhaba wa mafuta ya kula nchini.

Akizungumza wakati wa maonesho ya tatu ya SIDO Kitaifa yanayoendelea mkoani Wilayani Kasulu mkoani Kigoma  Meneja wa Kituo cha Uwekezaji nchini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Venence Mashiba amesema tayari kituo hicho kimefanya tafiti mbalimbali dhidi ya zao la michikichi na fursa zake, hivyo hatua inayofuata ni kutafuta wawekezaji ili kupandisha thamani ya zao hilo.

"Tumefanya tafiti kwenye zao la Mchikichi ambapo tumeangalia fursa zilizopo kwenye zao hilo ikiwa kuanzia kwenye uwekezaji wa kilimo cha Mchikichi , uwekezaji kwenye usindikaji wa bidhaa zinazotokana na zao hili, baada ya kumaliza utafiti wetu sasa tunaingia hatua ya pili ya kutafuta wawekezaji.Hivyo haya maeneo yote tunayafanyia mkakati wa makusudi kutafuta viwanda vikubwa au wawekezaji wakubwa ambao wanaweza kuja kuwekeza mkoani Kigoma au katika haya maeneo,"amesema Mashiba.

Kuhusu ushiriki wa TIC kwenye maonesho hayo, amefafanua lengo lao ni kutoa elimu kwa umma pamoja na kuwaunganisha wajasiriamali wadogo na fursa mbalimbali ili waweze kujikwamua kiuchumi."Tunatoa elimu kwa umma lakini tunatoa elimu kuhusu shughuli tunazofanya, hasa katika kuwasaidia au kuwawezesha wawekezaji pamoja na wajasiriamali wadogowadogo ambao ndio walengwa wa maonesho haya."

Kwa upande wao baadhi ya wakulima wa zao la Mchikichi mkoani Kigoma wamepongeza hatua ya TIC kuanza kutafuta viwanda vya kuchakata mafuta ya mawese kwani hatua hiyo itawezesha kuwanufaisha na kuongeza uzalishaji zaidi. "Ni nguvu za Serikali kutuwezesha , tunaweza kulima heka nyingi lakini tatizo ni la uwezeshaji, hivyo tuaomba serikali kutupa uwezo wa kilimo hiki cha Mchikichi ambacho kina gharama ya upandaji."

Aidha wamesema wameona namna ambavyo Serikali inaamini wakulima wa Kigoma wanaweza , hivyo wameiomba Serikali kuendelea kuweka msisitizo kwenye zao hilo .


Sehemu ya washiriki wa maonesho ya tatu ya SIDO kitaifa yanayoendelea wilayani Kasulu mkoani Kigoma wakifuatilia hotuba za viongozi kuhusu hatua zinazochukuliwa kuinua zao la Mchikichi

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...