Raisa Said,Handeni.
Mwenyekiti wa Handeni Mji mkoani Tanga Mussa Mkombati amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kuwapelekea fedha nyingi katika Miradi ya maendeleo iliyopo ndani ya mji huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Samia Cup alisema kuwa kitendo cha kuanzisha ligi hiyo nikurudisha fadhira kwa Kiongozi wa nchi aliyewasaidia katika Miradi ya maendeleo .
Mkombati alisema Serikali ya Awamu ya sita inafanya kazi kubwa katika suala zima la kusukuma maendeleo katika jamii jambo ambalo alieleza ni lazima waiunge mkono ili izidi kuwaletea bajeti kubwa katika Miradi hiyo.
" Sisi watu wa Handeni Changamoto yetu kubwa ni maji lakini tangu Serikali ya Awamu ya sita iingie madarakani tumepewa visima 15 vyenye thamani ya sh .Milion 345 na mradi mkubwa wa maji kata ya malezi wenye thamani ya Milion 248" Alisema Mwenyekiti huyo
Alisema kuwa mbali na kupata visima lakini pia wamepewa mradi mkubwa wa bwawa la Kwenkambala lenye ukubwa wa viwanja vitatu vya mpira lenye thamani ya sh billion 1.96 na pia ukarabati wa bwawa la chanika ambalo linasaidia kwasasa kutoa maji ambao unaendelea wanaamini miradi hiyo itakapokamilika itasaidia kupunguza changamoto hiyo ya muda mrefu.
Mkombati alieleza pia Kuna mradi mkubwa wa maji wa miji 28 wenye thamani ya bilion 380 mji wa handeni ni Mmoja wapo nakwamba endapo miradi yote ikikamilika itakamilisha ndoto ya Rais ya kumtua mama ndo kichwani hivyo mji handeni utakwenda kupata maji safi na salama.
Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa wakati wa majumuisho ya ziara ya Waziri wa Maji hivi karibuni katika kata ya mabanda,Waziri aliahidi kutoa Milion 671 ili zisaidie kutoa maji konje kupeleka mabanda na zitasaidia kununua pampu za maji ili zisaidie kukarabati mradi wa HTM uliopo.
Awali akizindua ligi hiyo itayozikutanisha kata zote 12 za mji huo na mitaa yote 60 ,Mbunge wa Jimbo hilo Ruben Kwagwilwa Alisema kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kutaka kufikisha Asante kwa Rais kwa kuwapatia upendeleo wa kuwapa Miradi mikubwa na ya kipekee katika mji wao.
Kwagilwa Alisema kuwa tangu dunia iumbwe mji wa handeni haujawahi kuwa na taa za barabarani lakini kipindi hiki inawaka.
Hata hivyo Mbunge huyo Alisema licha ya kufikisha Asante kwa Rais kupitia ligi hiyo lakini pia ni sehemu ya utekelezaji wa ilani na ahadi alizozitoa wakati akipita kuomba kura kipindi cha kampeni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...