Na Amiri Kilagalila,Njombe
Wananchi
wa Lutala kijiji cha Mbongo wilayani Ludewa mkoani Njombe wanaomba
kukopeshwa mashine ya kusaga na kukoboa nafaka ili kurahisisha kazi
kubwa wanayoifanya kwa kusaga nafaka kutumia mawe na vinu ili kupata
unga kwa ajili ya matumizi ya chakula na lishe kwa watoto.
Wito
umetolewa na wananchi hao wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo hilo
wakili Joseph Kamonga alipofika na kueleza shughuli mbali mbali na
utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa.
John
Edward (Mlope),Rosaria Haule na Angeus Mkinga ni miongoni mwa wananchi
wa Lutala wamesema kwa miaka yote wamekuwa wakitumia vinu na mawe katika
kusaga nafaka huku wengine wakisafiri umbali mrefu kupata huduma ya
mashine.
“Siku zote
tunatwanga mahindi kwa mkono kwenye vinu tunapata shida kwa kuwa hatua
zake ni ngumu na ukitaka kufuata mashine basi lazime ubebe nafaka
kichwani na kuenda maeneo mengine umbali wa masaa matatu”alisema Rosaria
Haule
John Edward
Alisema “Lutala tunakikundi kinaitwa tupendane chenye wanachama 34
tunaomba tukopeshwe mashine,sahizi tunaenda kusaga Iwela wengine wako
Nsungu na wengine Mbongo hili tunaomba tusaidiwe sana”
Kwa
upande wake mbunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Joseph
Kamonga,ameiomba ofisi ya maendeleo ya jamii kuwawezesha kikundi hicho
kiweze kukidhi vigezo na kupatiwa mkopa ili kuwapunguzia changamoto ya
kusafiri umbali mrefu.
“Niombe
afisa maendeleo ya jamii hii mashine hapa ipatikane kwasababu watu
wanasafiri kilomita nyingi sana kwenda kusaga ni bora tuwakopeshe ili
waondokane nahii adha”alisema Kamonga.
Baadhi ya akina mama wa Lutala wakigaagaa chini kuonyesha ishara ya shukrani kwa mbunge wa jimbo hilo mara baada ya kuomba maendeleo ya jamii kupitia halmashauri kuwakopesha mashine ya kusaga na kukoboa nafaka ili kuwapunguzia changamoto.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akizungumza na wananchi wa Lutala namna ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyoendelea kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la Ludewa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...