Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba amewahimiza Watanzania kuchangamkia fursa zinazokuja na mradi wa EACOP kwa kujiandaa mapema kuhakikisha fursa hizo zinawanufaisha. Waziri Makamba ameyasema hayo katika warsha maalumu ya ushiriki wa Wazawa iliyofanyika Jijini DSM na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo wawakilishi wa wawekezaji wa EACOP (Total Energies na TPDC), Wabunge, Wakandarasi wakubwa wa mradi (level one contractors) na wafanyabiashara wa Tanzania.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha hiyo, Waziri Makamba alisema “ Serikali imehakikisha Wazawa wananufaika na mradi huu kwa kutenga huduma na bidhaa mahususi ambazo ni lazima zitolewe na Wazawa, lengo likiwa ni kutoa kipaumbele kwa Wazawa kunufaika na mradi huu”.  

Waziri Makamba pia alieleza Serikali imewekeza kimkamkati katika mradi wa EACOP ambapo TPDC inashiriki kwa asilimia 15% na tayari Serikali imeshaipatia TPDC shilingi Bilioni 259.96 ikiwa ni sehemu ua malipo ya ushiriki huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alisema kuna hatua mbali mbali za muhimu ambazo mradi imeshakamilisha ikiwemo malipo ya fidia kwa utwaaji wa ardhi maeneo ya kipaumbele ambapo takribani bilioni 2.28 imetumika kulipa watu 351.

Dkt. Mataragio aliongeza pia kuwa tayari kazi ya kutathmini na kuhakiki mali za wananchi 9,122 watakaopisha eneo la mkuza wa bomba imekamilika na hatua inayofuata ni kulipa ambapo Serikali italipa takribani Shilingi Bilioni 25.5.

Mkurugenzi wa TPDC aliongeza kuwa Serikali kupitia TPDC ndio atakuwa mmiliki wa mkuza na maeneo ya kipaumbele na kukodisha kwa kampuni ya EACOP ambayo itakuwa ikilipa kodi ya pango ambayo itakuwa ni chanzo kipya cha mapato kwa TPDC.

Warsha hii ya ushiriki wa wazawa ni muendelezo wa warsha mbali mbali zinazofanyika maeneo bomba litakapopita kwa lengo la kuwaandaa Wananchi kunufaika na fursa za mradi na kuupokea mradi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...