****************************************
WAZIRI Wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu,) Jenista Mhagama amesema Serikali kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF,) watahakikisha miradi yote ya nyumba za makazi inayosimamiwa na mfuko huo itakamilika ifikapo Agosti 2022 na hiyo ni pamoja na kukamilika kwa hosteli za wanafunzo wa vyuo vikuu na miundombinu katika miradi ya nyumba hizo zilizopo Toangoma, Mtoni Kijichi na Dungu mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi hiyo Waziri Mhagama amesema NSSF ikiwa mmoja ya mfuko unaosmamiwa na Serikali umekuwa ukitekeleza majukumu yake ya msingi makubwa kwa mujibu wa sheria ikiwemo kuandikisha wanachama, kukusanya michango pamoja na kuhakikisha malipo ya mafao kwa wastaafu yanalipwa kwa wakati na wamekuwa na miradi mbalimbali ya uwekezaji wa fedha za wanachama zinazoandaliwa katika ulipaji wa mafao ikiwemo mradi wa nyumba hizo za makazi.
Amesema, mradi wa nyumba hizo za makazi katika jiji la Dar es Salaam ni moja kati ya uwekezaji unaofanywa na mfuko huo uliowekeza katika nyumba za makazi katika maeneo ya Mtoni Kijichi, Toangoma na Dungu miradi yenye tija ambayo Serikali imekuwa ikiisimamia kwa ukaribu na kueleza kuwa baada ya kuikagua miradi hiyo mitatu ameridhishwa na utekelezaji wake.
"Katika nyumba za makazi za Mtoni kijichi ni moja ya ambalo zimetengwa hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu ninawaomba NSSF mhakikishe ukamilikaji wa miundombuni mhuhimu hasa barabara, taa za barabarani, fensi pamoja na huduma muhimu za afya kwa maana ya Zahanati kwa haraka zaidi ili kuweza kuwahudumia wakazi wa maeneo haya,'' Ameeleza Waziri Mhagama.
Aidha ameipongeza NSSF kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa malengo na matarajio yaliyokusudiwa na kuiagiza kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na Serikali na kukaa meza ya maridhiano na wakandarasi ili waweze kurejea kazini ili kukamilisha nyumba hizo ifikapo 2022 na kuwataka watanzania kutembelea, kupanga na kununua nyumba hizo za kisasa zinazosimamiwa na mfuko huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa NSSF Masha Mshomba amesema, mfuko huo umekuwa ukiendelea kutekeleza miradi hiyo kwa kushirikiana na Serikali kwa ukaribu zaidi na hadi kufikia Agosti 2022 itakuwa imekamilika kwa kiasi kikubwa na watatekeleza maagizo yaliyotolewa na Serikali kwa kuweka miundombinu muhimu itakayowavutia wapangaji ili kuweza kupata mapato ya kutosha yatakayotunisha mafao.
Amesema,watashirikiana na Serikali kwa ukaribu zaidi katika kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za afya na kuwataka wananchi kutembelea nyumba hizo kwa huduma za kupanga na kununua kwa gharama nafuu.
Akizungumza katika ziara hiyo mkazi wa nyumba za makazi Dungu Flora Mwekipesile amesema makazi hayo yaliyopo pembezoni mwa bahari ni mazuri na yanaridhisha na wanapata huduma zote za muhimu na kuiomba Serikali kusafisha maji ya chumvi katika eneo hilo jambo ambalo Waziri Mhagama ameiagiza Menejimenti ya NSSF kulitatua kwa haraka na kuwataka wakazi hao kupanda miti na maua ili kupendezesha mazingira.
Vilevile Mwenyekiti wa eneo la nyumba za makazi za NSSF Toangoma Emmanuel Keffa amesema, mazingira ya makazi na tulivu na safi kabisa na ameemwomba Waziri Mhagama barabara itakayounganisha nyumba za NSSF Toangoma na nyumba za makazi NSSF Mtoni Kijichi ili kuongeza thamani ya miradi hiyo jambo ambalo Waziri Mhagama ameeleza kuwa huduma za msingi na endelevu litaangaliwa kwa kuhakikisha huduma za msingi zinafika katika eneo hilo ikiwemo miundombinu na kituo cha polisi na kuwataka NSSF kutoa mrejesho wa kila jambo kwa viongozi wa maeneo hayo hasa wenyeviti.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...