Na Shukrani Kawogo, Njombe
Imeelekezwa kuwa serikali hutumia zaidi ya bilioni 54.4 kila mwaka kwaajili ya kuagiza dawa kutoka nje ya nchi ili kusaidia wagonjwa katika Hospitali mbalimbali hapa nchini kitu ambacho kimepelekea serikali kuwekeza katika mradi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa (msd) ili kuokoa fedha hizo.
Akizungumza hayo mbele ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM)Taifa waziri wa afya Dk. Dorothy Gwajima walipofanya ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa hizo kilichopo katika mji wa Makambako kijiji cha Idofi mkoani Njombe amesema kiwanda hicho kitakapokamilika kitaokoa zaidi ya bilioni 33 ambazo kwa sasa zinapotea.
Ameongeza kuwa kiwanda hicho kitazalisha dawa za magonjwa mbalimbali ambazo zitatua tatizo la upungufu wa dawa hapa nchini kwa asilimia 100% pamoja na groves ambazo zitasaidia kupunguza tatizo kwa asilimia 86 %.
"Nchi yetu imekuwa ikikumbwa na upungufu mkubwa sana wa dawa na groves hasa katika kipindi hiki cha Corona kumekuwa na uhitaji mkubwa wa gloves lakini zimekuwa zikipatikana kwa uchache hivyo kiwanda hiki kitatufanya tupate dawa zenye ubora zaidi kwakuwa dawa tunazoziagiza mara nyingine zinakuja huku zikiwa zimebakiza muda mchache kuharibika", amesena Dk. Gwajima.
Pia ameishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha za ujenzi wa mradi huo kiasi cha shilingi bilion 18 ili kufikisha ujenzi huo kwa hatua iliyofikiwa lakini wataalam wa sekta ya afya kupitia msd pamoja na wananchi wa makambako kwa kutumia force account wametumia bilioni 12 badala ya bilioni 18.
Aidha kwa upande wa katibu mkuu wa CCM taifa Daniel Chongolo amewapongeza idara ya afya na kusema kuwa uwepo wa kiwanda hicho ni mapinduzi makubwa ambapo ajira zaidi ya 350 za watanzania zitaenda kupatikana sambamba na kuokoa fedha inayopotea.
Amesema kutokana na umuhimu wa kiwanda hicho watahakikisha kinamalizika kwa gharama yeyote ile hata zikitakiwa fedha za kuongezea ni lazima zitolewe ili kuhakikisha kiwanda hicho kinaendelea na kuanza kufanya kazi.
Sanjali na hayo pia amefurahishwa kuona wafanyakazi waliopo katika ujenzi huo kwa asilimia kubwa ni watanzania na mgeni mmoja tu kitu ambacho kinapelekea watanzania hao kupata ujuzi ambao watautumia kwa maendeleo ya taifa.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Eng. Marwa Rubirya akizungumza katika mkutano wa hadhara baada ya ukaguzi wa kiwanda cha dawa cha msd uliofanywa na katibu mkuu wa CCM taifa sambamba na waziri wa afya Dk. Dorothy Gwajima.
Viongozi mbalimbali wakiwa wamesema kuwasalimia wananchi pamoja na wanachama wa CCM baada ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa cha msd unaoendelea latika mji wa Makambako kijiji cha Idofi. Kutoka kushoto ni mkuu wa mkoa wa Njombe Eng. Marwa Rubirya, waziri wa afya Dkt. Dorothy Gwajima, katibu mkuu wa CCM taifa Daniel Chongolo pamoja na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Mwamwala.
Waziri wa afya Dkt. Dorothy Gwajima akiwa sambamba na katibu mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo wakiangalia baadhi ya mitambo ya kutengenezea dawa katika kiwanda cha dawa kilichopo katika mji wa Makambako kijiji cha Idofi mkoani Njombe
Waziri wa Afya Dk. Dorothy Gwajima akizungumza baada ya ukaguzi wa kiwanda cha dawa cha msd kilichopo katika mji wa Makambako mkoani Njombe.
Wanachama wa CCM wakiwa sambamba na viongozi wao pamoja na waziri wa afya Dkt. Dorothy Gwajima wakikagua ujenzi wa kiwanda cha dawa cha msd
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...