Na Zainab Nyamka, Michuzi TV

Licha ya kutokukuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, na kushika nafasi ya Pili Klabu ya Yanga imeongoza mapato ya mlangoni na kuwaacha mbali watani zao wa jadi.

Yanga imekuwa kinara kwa timu 18 zilizoshiriki msimu wa Ligi Kuu 2020/21 na mbili zilizocheza Michezo ya Play Off kwa kupata jumla ya Shiling Milion 986 akifuatiwa na Simba mwenye Milioni 929.

Mbali na hilo, Yanga pia wameibuka kinara kwa kuwa timu iliyoingiza mashabiki wengi kwa msimu wa 2020/21 ambapo takribani ya wananchi 141,861 huku Simba wakiingia mashabiki 131,518.

Kwa upande wa Viwanja, Uwanja wa Benjamin Mkapa umeweza kuingiza mashabiki 274, 273 huku Jamhuri Dodom ukiinguiz watu 52,467

Upande wa mapato, Uwanja wa Benjamin Mkapa umeingiza Kiasi cha Bilion 1.8 ukifuatiwa na Jamhuri Dodoma ukipata Milion 287

Timu ambayo iliingiza mashabiki wachache katika mechi zao ni  Namungo wakipata Milion 32.4 kama mapato ya msimu mzima na Kwa upande wa  Viwanja, CCM Gairo Morogoro ukipata Shiliing 195,000


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...