Na Mwandishi Maalumu, Arusha.
ZAO
jipya la Utalii wa mchezo wa gofu uliozinduliwa mapema 25 Septemba
mwaka huu Jijini Arusha, kuongeza idadi ya Watalii nchini kama ilani ya
Chama cha Mapinduzi (CCM ) ilivyoelekeza, Wizara ya Maliasili na Utalii.
Hayo
yamebainishwa Jijini hapa na, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas
Ndumbaro ambapo pia amesema juhudi kubwa za kimkakati zilizoendeshwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan
kupitia Royal Tour, zimeweza kuchagiza ubunifu wa kimkakati katika
Wizara hiyo ili kwenda sambamba na maono ya Mhe.Rais ya kuongezeka
idadi ya watalii nchini.
''Mimi
kama Waziri pamoja na Watendaji wote katika Wizara ninayoiongoza
shabaha yetu kubwa ni kuona idadi ya watalii inaongezeka kwa kuibua na
kubuni mazao ya utalii ambayo ni mapya hapa kwetu" alisisitiza Dkt.
Ndumbaro
Aidha, Dkt.
Ndumbaro amemshukuru kwa mara nyingine Mhe Rais kwa kuonesha njia
katika sekta hiyo na wao kupitia wizara ya Maliasili na Utalii
kilichobaki ni utekelezaji ikiwemo kuanzia pale Mhe.Rais alipoishia.
Kwa
upande wake, Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala
ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa Utalii kupitia
mchezo wa gofu wa siku mbili 25-26 Septemba, unaofanyika katika viwanja
vya Kiligolf Jijini hapa, amesema mchezo huo unaowakutanisha watu
kutoka mataifa mbalimbali duniani ambao huja kwa ajili ya kucheza na
kuongezeka pato litokanalo na utalii.
"Kwetu
sisi nchini Kenya mchezo wa gofu umekuwa na mwamko mkubwa na tumekuwa
na mashindano makubwa yanayowakutanisha washiriki kutoka mataifa
mbalimbali duniani kila mwaka" alisisitiza Waziri Mhe. Najibu Balala.
Ameongeza
kuwa, uzinduzi huo wa mchezo wa gofu utachochea watalii kukaa kwa muda
mrefu nchini kwa vile watalii watakuja kwa ajili ya kuona wanyamapori
lakini pia wataongeza siku ya zaidi ya siku mbili kwa ajili ya kucheza
mchezo huo.
Amesema
mpango wa nchi ya Kenya ni kutaka kuona Tanzania inafanikiwa
kufungamanisha michezo na utalii ili ziweze kushirikiana ambapo
wachezaji wa gofu watakaocheza Kenya waje pia kucheza mchezo huo nchini
Tanzania.
Waziri Mhe
Balala amesema mkakati huo endapo utaweza kufanikiwa utasaidia kuongeza
idadi ya watalii na kupunguza utegemezi wa kufikiria kuwa utalii pekee
ni ule wa kuona wanyamapori pekee yake.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Bodi yaTaifa ya Utalii ( TTB) Jaji ( Mst)
Thomas Mihayo amesema uzinduzi wa utalii wa gofu umekuja wakati muafaka
ambapo Mhe.Rais amekuwa akionesha njia na kuita Wawekezaji kutoka nchi
za nje kuja kuwekeza nchini.
"Leo
hii Mataifa 13 yameshiriki na tunaamini Washiriki hawa watakaporudi
nchini kwao watakuwa mabalozi wazuri mbali ya kueleza walivyoshiriki
katika mchezo huo bali wataelezea uzuri wa Tanzania" alisema Jaji
Mihayo.
Kwa upande wake,
Martin Kiula ambaye ni mshiriki wa mchezo huo amewatoa wasi wasi watu
wanaoshindwa kujifunza mchezo huo wakifikiria kuwa mchezo huo ni maalum
kwa ajili ya watu matajiri pekee.
Katika
uzinduzi huo jumla ya Wachezaji ambao ni watalii 140 kutoka nchi 13
duniani wameshiriki na wanatarajia kukaa nchini kwa zaidi ya siku tano
ikiwa ni mkakati wa kuongeza idadi ya Watalii kutoka milioni 1.5 hadi
kufikia watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025
Uzinduzi
huo wa Utalii kupitia mchezo wa Gofu unatarajiwa kufikia tamati leo 26
Septemba kwenye viwanja hivyo vya Kiligolf, Jijini hapa Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii,
Dkt.Damas Ndumbaro akiwa amepiga mpira wa gofu huku akifuatilia muelekeo
wa mpira huo huku washiriki wakishuhudia mara baada ya mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala kuzindua utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo mefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( wa pili kushoto) akiwa
kwenye picha pamoja na Wachezaji waenzake wa mchezo wa gofu mara baada
ya mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya,
Mhe.Najib Balala kuzindua utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la
utalii nchini, uzinduzi huo umefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu
Jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ( kulia) akimuonesha mgeni rasmi Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala baadhi ya hoteli zilizopo katika uwanja wa Gofu wa Kiligofu mara baada ya kuzindua
utalii huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo
mefanyika jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza na Wachezaji wenzake mchezo wa gofu mara baada ya mgeni rasmi Waziri
wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya, Mhe.Najib Balala kuzindua utalii
huo wa gofu ambalo ni zao jipya la utalii nchini, uzinduzi huo mefanyika
jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha, Wengine ni Viongozi
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Taasisi zilizo chini ya
wizara hiyo. Waziri wa Utalii na Wanyamapori
wa Kenya, Mhe.Najib Balala akizindua utalii wa gofu ambalo ni zao jipya
la utalii nchini huku akiwa anashuhudiwa na Washiriki mbalimbali wa
mchezo huo kutoka ndani na nje ya nchi katika uzinduzi huo uliofanyika
jana katika viwanja vya Kiligofu Jijini Arusha.Wa tatu kulia ni Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...