Benki ya Exim Tanzania, mwishoni mwa wiki iliandaa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wake mkoani Iringa ili kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Akizungumza kwenye hafla hiyo iliyohudhuliwa na wadau mbalimbali wa benki hiyo wakiwemo viongozi wa kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu alisema, kupitia hafla hiyo walilenga pia kutoa fursa miongoni mwa wateja hao ili waweze kufahamiana na kufungua wigo wa kufanya biashara pamoja.
“Pamoja na kushukuru kwa namna ambayo wateja wetu wamekuwa nasi hadi kufikia mafanikio ya ukuaji na ubora wa huduma zetu, hafla hii inatoa fursa kwa wateja wetu pia kufahamiana wao kwa wao na hivyo kufungua milango ya fursa baina yao,’’ alisema Matundu.
Alisema hali ya uchumi katika mkoa huo inatoa fursa kubwa ya ukuaji kwa benki hiyo na hiyo ndio sababu imejipanga kuhudumia wateja Wakubwa, Wadogo na wa Kati ili kuleta ustawi kwenye sekta muhimu kwa mkoa huo ikiwemo biashara, kilimo na ufugaji .
“Takwimu zinaonyesha Mkoa wa Iringa umeendelea kujenga uchumi imara na endelevu, na hivyo ufanisi katika mfumo wa fedha ni moja ya mahitaji ya muhimu na ya msingi katika ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla. Benki ya Exim tumejipanga kuhakikisha tunafanikisha hilo pamoja ’’ alisema
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Bi Queen Sendiga, Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Bw Ephraim Kyando pamoja na kuipongeza benki hiyo kwa huduma zake bora mkoani humo aliuomba uongozi wa benki hiyo kuangalia namna kujitanua zaidi mkoani humo kwa kuongeza matawi zaidi kwenye wilaya mbalimbali za mkoa huo ili huduma zake ziweze kuwanufaisha wananchi wengi wa mkoa huo.
“Binafsi nimekuwa nikikoshwa sana na namna benki ya Exim inavyoweza kutoa huduma zake ikiwemo mikopo kwa wateja wake bila uwepo wa misuguano kwenye marejesho ya mikopo husika…hii tafsiri yake ni kwamba mpo makini kwenye utoaji wa huduma zenu na hicho ndio kitu kinachowasaidia kuepuka migogoro na wateja wenu…hongereni sana,’’ alisema.
Awali akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo alisema benki hiyo imejipanga zaidi kwa kuboresha mifumo na taratibu za utoaji huduma ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja na soko, kuongeza weledi na umahiri wa wafanyakazi pamoja na kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa itakayowezesha kuwafikia wateja wengi zaidi, kwa urahisi zaidi, mahali popote walipo na hivyo kuwaondolea ulazima wa kutembelea matawi ya benki hiyo pindi wanapohitaji huduma
“Tumejipanga kuahakikisha Benki inafanya vizuri kwa kuweka kipaumbele katika uboreshaji wa namna ya kupata na kutumia huduma zetu. Tunataka upatikanaji na utumiaji wa huduma za Benki ya Exim uwe rahisi, huku tukiendelea kusizogeza huduma hizo karibu zaidi na wateja wetu.’’ Alisema.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wateja wengine wa benki hiyo Bi Atu Jonas pamoja na kuonyesha kuridhishwa na huduma za benki hiyo aliiomba benki hiyo izidi kujitanua mkoani humo ili huduma zake ziweze kuwafikia na wananchi wengine mkoani humo hususani wafanyabiashara na wakulima wanaohitaji huduma bora za kibenki.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1997 benki hiyo imezidi kujitanua ndani na nje ya nchi ambapo ambapo hadi sasa benki hiyo imefanikiwa kufungua matawi yake kwenye nchi za Uganda, Ethiopia, Comoro na Djibouti
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (katikati) akisalimiana na wateja mbalimbali wa benki hiyo mkoa wa Iringa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo (Kulia) na Meneja wa Benki hiyo tawi la Iringa Bw Michael Richard (Kushoto)
Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Bw Ephraim Kyando akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mbunge wa Iringa Mjini Bi Jesca Msambatavangu akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mkuu wa Huduma ya Rejareja wa Benki ya Exim, Andrew Lyimo akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Iringa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mbunge viti maalum Mkoa wa Iringa, Mh Ritta Kabati akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa na Benki ya Exim kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Akitoa shukrani kwa niaba ya wateja wengine wa benki hiyo Bi Atu Jonas (Pichani) pamoja na kuonyesha kuridhishwa na huduma za benki hiyo aliiomba benki hiyo izidi kujitanua mkoani humo ili huduma zake ziweze kuwafikia na wananchi wengine mkoani humo hususani wafanyabiashara na wakulima wanaohitaji huduma bora za kibenki.
Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim, Agnes Kaganda akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Iringa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (Kushoto) akizungumza na wateja wa benki hiyo mkoa wa Iringa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Iringa iliyolenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...