CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka bodi ya mikopo ya wanafunzi elimu ya juu nchini (HESLB) kuendelea kuweka utaratibu mzuri zaidi wa kuendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali pamoja na kutoa elimu ya uelewa juu ya namna sahihi ya kutuma maombi kwa wanafunzi wanaotaraji kujiunga na elimu ya juu ili kuweza kuepuka makosa yanayowanyima fursa ya kunufaika na mikopo hiyo.

Hayo yameelezwa Leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, alipotembelea HESLB kuona jinsi inavyofanya kazi.

Shaka alieleza kuwa, Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ibara ya 80 (h) inasema serikali itaimarisha na kuboresha mfumo wa ugharimiaji wa elimu ya juu ikiwemo bodi ya mikopo ya Juu, ili kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wenye uhitaji na sifa stahiki wanapata fursa ya kujiunga na elimu ya juu.

Alisema Rais Samia ameonyesha dhamira ya dhati kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa ya kusoma ambapo, ameongeza mkopo wa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka sh bilioni 464 hadi sh. bilioni 570.

Aidha ndg Shaka ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kinaridhishwa na namna bodi hiyo inavyotekeleza majukumu yake huku akisema kwa haya yaliyofanyika Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha na kuthibitisha kwa vitendo kuwajali vijana wakitanzania wanaotoka familia maskini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...