Kampuni ya simu ya Halotel na wafanyakazi wake leo wamewatembelea watoto wenye changamoto ya kiafya ya vichwa vikubwa na mgongo wazi pamoja na wazazi/walezi wao waliolazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya kusheherekea nao pamoja katika kuadhimisha miaka 6 ya kampuni hiyo na utowaji wa huduma za mwasiliano na kuwaletea mahitaji mbalimbali ya kijamii kama sehemu ya msaada wao kama wafanyakazi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo Naibu Mkurugenzi wa Halotel, Thang Bui Van, akiwa pamoja na Afisa Mahusiano ya nje Halotel Bw. Yassir Matsawily amesema kuwa katika kuhakikisha tunasaidia sekta hii ya afya nchini, tumeona ni vyema kuendeleza fursa hii ya kuja kuwatembelea watoto hawa na kusherehekea nao kwa kuwapa misaada hii ya kijamii ili waweze kuimarika kiafya wanapoendelea kupata matibabu wodini hapa. Hii ni pamoja na kuonesha upendo kwao na kutambua thamani yao katika jamii ya watanzania.
“Tunatambua changamoto mbalimbali ambazo ziko katika kuwapa matibabu watoto wenye matatizo ya kiafya ya vichwa vikubwa na mgongo wazi wawapo wodini wakisubiri kupata matibabu ya upasuaji hivyo katika kujali na kutambua thamani ya afya zao tumeona ni vyema tukawaletea mahitaji haya muhimu ya kuimarisha afya zao aliongeza Yassir”
Akiongea baada ya kukabidhiwa msaada huo, kwa niaba ya wazazi wengine wodini hapo bi Rose Vincent alisema, “Tunajisikia furaha sana kukumbukwa na kampuni ya simu Halotel na kupokea msaada huu kutoka kwao, tumefarijika sana na tunaomba waendelee na moyo huu huu wa kuisaidia jamii ya watanzania”
Kwa upande wa Uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Afisa Uhusiano Bw.Patric Mvungi alisema “Tumefarijika sana kwa kupokea msaada huu kutoka Kampuni ya simu ya Halotel na wafanyakazi wake, tunawashukuru sana kwa kuthamini afya za watoto hawa lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kuisaidia sekta ya afya nchini. Hii ni hatua mpya na kubwa na imekuwa endelevu kwetu sisi katika kuimarisha ushirikiano wetu na Halotel kwa kiwango cha juu hasa katika kuboresha sekta ya afya kwa ujumla”.
Mmoja wa wazazi Rose Vincent katika Taasisi ya Tiba na Mifupa Muhimbili (MOI) akitoa shukrani kwa Wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel kwa kuwakumbuka na kuwaletea mahitaji mbalimbali ya muhimu ya kijamii abayo yata wasadia sana pindi wanapopata matibabu hospitalini hapo.
Afisa Mahusiano ya nje wa Halotel Yassir Matsawily akiongea na waandishi wa habari leo, baada ya kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali ya kijamii kwa watoto na wazazi walioko katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipowatembelea na kuwapelekea mahitaji hayo ikiwa ni katika kuadhimisha miaka sita ya utoaji wa huduma za mawasiliano hapa nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...