NA MWANDISHI WETU
MEYA wa jiji la Dar es salaam, Omary Kumbi la Moto amesema kwamba Beach ya Dengu itakuwa  kivutio kikubwa cha utalii kwa wazawa na wageni watakaofika jiji la Dar es salaam.

Hayo aliyasema Jana alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa ufukwe huo ambao umepewa jina la 'Ilala canival' uliopo eneo la Ilala. Akizungumzia kuhusu ufukwe huo, Meya Kumbi la Moto alisema kuwa Jana ilikuwa ni utambulisho ambao umewapa watu fursa ya kufanya ziara ya kujua historia na vivutio vya jiji la Dar es salaam.

"Kwa kutumia basi letu la utalii wananchi wamezunguka katika vivutio vya jiji bila kulipa chochote. Na uzinduzi huu hautakuwa wa mwisho Bali utakuwa ukifanyika Kila baada ya miezi mitatu kuhamasisha watu kuja kupumzika." alisema Meya huyo.
Akizungumzia kuhusu lengo la ufukwe huo alisema ni kupumzika bure na wala jiji halina Mpango wa kuufanya kuwa chanzo chake cha mapato. Kuhusu usalama alisema wanampango wa kujenga kituo Cha Polisi na pia Kutakuwa na doria inayofanyika mara kwa mara.

Katika suala la kulinda usafi alisema vitajengwa vyoo vya kisasa ili watalii na wenyeji watakaofika waweze kuvitumia.
Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan Zungu, alisema uzinduzi wa ufukwe wa Dengu utasaidia kutangaza utalii wa ndani ya jiji la Dar es salaam.
Anafuraha kuona namna uzinduzi huo ambao ulipewa jina la 'Ilala canival' kufana kutokana na kutoa fursa ya watu kuchanja bure ili kujilinda na maambukizi ya Uviko 19.

Aliongeza kuwa ufukwe huo utasaidia kuwaondoa watu kupumzuka katika baa na kuhamia hapo kupata mapumziko na familia zao.Alitaja faida nyingine kuwa ni kuwaruhusu wafanyabiashara ndogondogo kufanyashughuli zao kwa lengo la kujiingizia kipato na kujiinua kiuchumi.

Mkuu wa maudhui wa Clouds Media Group (CMG), Sebastian Maganga, alitumia nafasi hiyo kushukuru jiji la Dar es salaam, kuwatunuku uratibu wa Ilala carniival.
 mwisho.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...