Na.WAMJW-MAFINGA

Halmashauri ya MAFINGA wanaendelea na uhamasishaji wa chanjo DHIDI ya UVIKO-19 kwa Wananchi wa Wilaya  hiyo.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji MAFINGA Dkt.Innocent Mhagama amesema kuwa Halmashauri hiyo imejipanga Katika kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo Kwenye shughuli zao za Kila siku.

"Kama Halmashauri tunaendelea kuhamasisha Kwenye Mitaa yetu ikiwemo maeneyo ya makazi,mtaa kwa mtaa ili kuhakikisha wananchi wanaelewa.

Aidha, Dkt Mhagama amesema Katika kutekeleza Mpango wa Jamii Shirikishi na Harakishi  na Harakishi wa uhamasishaji dhidi ya chanjo ya UVIKO-19 wameweza kukutana na wafanyabiashara wote wa Mji na wameweza kuwapatia elimu na kuwajibu maswali yaliyokuwa yakiwatatuza hapo awali.

Ameongeza kuwa wananchi wengi walikua na maswali ambayo walikua na taarifa potofu kuhusu Chanjo hizo na ziliwafanya wasiweze kuchanja Ila kwa elimu waliyowapatia wameelewa na wamehamasika kuchanja.

Dkt.Mhagama amekiri kwamba awali muitukio ulikua ni Mdogo Ila baada ya kutoa elimu kila mahali wananchi wameweza kujitokeza na kuchanja kwa wingi.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...