Muonekano wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wavula Nachingwea ambayo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliweka jiwe la msingi la ujenzi wake, Oktoba 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Kaimu Mhandisi wa wilaya ya Nachingwea, Misoji Sahani ambaye alitoa maelezo kuhusu michoro ya Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana Nachingwea kabla ya Waziri Mkuu kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Oktoba 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Kaimu Mhandisi wa wilaya ya Nachingwea, Misoji Sahani (Kulia) baada ya kuvutiwa ubora na viwango vya hali ya juu vya ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana Nachingwea ambayo ujenzi wake umesimamiwa na Mhandisi huyo. Mheshimiwa Majaliwa pia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo, Oktoba 25, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Sekondari Maalum ya Wavulana Nachingwea, Oktoba 25, 2021. Kulia ni Mbunge wa Nachingwea , Dkt. Amandus Chingwile na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...