Na Mwandishi wetu

Dar es Salaam. Mashindano ya kuogelea ya Kanda ya Nne Afrika (Cana Africa Zone 4) yameanza kwa kushindo jijini Dare s Salaam huku waogeleaji wa Tanzania wakionyesha makali yao.

Mashindano hayo yanafanyika kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), Masaki yanashirikisha waogeleaji wa Tanzania zaidi ya 70.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya kuogelea, Alexander Mwaipasi alisema kuwa mashindano hayo yanashirikisha nchi zaidi ya 20 na amevutiwa na maendeleo ya waogeleaji wa Tanzania mpaka sasa.

Mwaipasi alisema kuwa waogeleaji wa Tanzania wameonyesha uwezo mkubwa na wanatarajia kupata matokeo mazuri mara baada ya kumalizika kwake.

Alisema kuwa wachezaji  wengi wa Tanzania wameweza kupunguza muda wao wa kuogelea (PBs) na kuleta matumaini makubwa ya kukusanya pointi nyingi.

“Mpaka sasa nimevutiwa na ushindani wa waoegeaji wa Tanzania pamoja na ukweli kuwa wanashindana na waogeleaji wa nchi nyingine zaidi ya 20. Tutarajie matokeo mazuri na tunaamini kuwa tutafanya vizuri,” alisema Mwaipasi.

alisema kuwa wanashindana na nchi mbalimbali ambazo ni Afrika Kusini, Zambia,  Burundi,  Ethiopia,  Kenya,  Rwanda,  Sudan na Uganda.

Pia kuna nchi kama Angola, Botswana, Comoros, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, Eswatini  na Zimbabwe.

Kwa mara ya kwanza, mashindano hayo yanaonyeshwa live kupitia Champion Rise televisheni kupitia link; https://www.youtube.com/watch?v=KXWrnXVNQE4 na hakuna mashabiki kutokana na zuio la ugonjwa wa Uviko 19.




 Mashindano ya kuogelea la Kanda ya nne yaanza kwa vishindo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...