Na John Walter-Hanang
MBUNGE wa Hanang ameupiga Mwingi sana na kusepa na Kijiji, ndivyo unavyoweza kusema kwa jinsi Mamia ya watu walivyofurika katika uwanja wa Katesh kushuhudia fainali ya Mashindano yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Hanang Mhandisi Samwel Hhayuma aliyoyapa jina la Mlima maarufu wilayani humo (Mountain Hanang Cup).

Katika Mashindano hayo yaliyodumu zaidi ya Mwezi Mmoja, Kata 32 kati ya 33 zilishiriki isipokuwa kata ya Balangdalalu pekee kwa sababu ambazo hazijafahamika.

Akifunga Mount Hanang Cup Mkuu wa wilaya ya hiyo Janeth Mayanja amempongeza Mheshimiwa Hhayuma kwa kuwawezesha vijana kuonesha vipaji vyao kwa kuwa kwa sasa michezo ni ajira na kuwataka wengine kuiga mfano huo.

Mbunge wa Jimbo la Hanang Mhandisi Samwel Hhayuma amewataka vijana kuthamini michezo kwa kuwa michezo kwa sasa imekuwa ni ajira ya kudumu ambayo inaweza kubadilisha maisha na kuwapatia vipato vikubwa na kwamba mashindano hayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka.

Aidha, amesema katika kipindi chake cha miaka mitano jimboni humo amedhamiria kutangaza utalii na kukuza uchumi wa wilaya ya Hanang na mkoa wa Manyara kwa ujumla kupitia sanaa, michezo na utamaduni.

Amesema Mlima Hanang ni mlima wenye kuvutia kutokana na mandhari yake nzuri inayopatikana katika kilele chake hivyo ni fursa ya kila mmoja ndani na hata nje ya nchi kufika kutalii katika mlima huo.

Mhandisi Hhayuma amewaasa vijana kuendelea kujituma na kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao hali itakayowasaidia kuepuka maradhi kushambulia miili yao na kuacha kukaa vijiweni bila kujishughulisha.

Katika michuano hiyo ya Mount Hanang Cup, kata ya Simbay imebeba Ubingwa na kukabidhiwa mkwanja mnono wa shilingi milioni moja, nafasi ya pili imeenda kwa kata ya Gitting ambayo imekabidhiwa laki saba na nusu huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na kata ya Katesh ambao wamekabidhiwa kitita cha milioni tano.

Michezo mingine ilikuwa ni riadha na netiboli kwa upande wa Wanawake ambao wote wamekabidhiwa zawadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...