Na Mwandishi Wetu, Iringa

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga amesema mkoa huo utaendelea kuipa thamani Sekta ya Misitu ili kuendeleza jitihada zake katika ukuaji wa Uchumi na Uwekezaji sambamba na kuhakikisha Sekta hiyo inachangia katika upatikanaji wa pato la Taifa.

Sendiga ameyasema hayo alipozungumza wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Uwekezaji kwenye Sekta ya Misitu litakalofanyika mkoani humo Novemba 10-12, 2021 katika viwanja vya Wambi, Mafinga.

Amesema kutokana na shughuli kubwa za Wananchi wa Iringa kuwa ni Kilimo, ameeleza wataendelea kusisitiza shughuli hizo ili kutoa mchango mkubwa kwenye mapato ya Serikali, ikiwa pamoja na kuwavutia Wawekezaji katika upandaji na uchakataji wa mazao yatokanayo na Misitu kama upatikanaji wa Mbao.

“Shughuli za upandaji miti katika mkoa wetu zilianza zamani, mwanzoni mwa miaka ya 1970, Serikali ilipoanzisha shamba la Saohil ambalo ndio shamba kongwe zaidi hapa nchini lenye ukubwa wa hekari 60,000. Mkoa wetu una kiu kubwa kuona uwekezaji katika misitu unakua na kuchangia zaidi katika pato la taifa. Kwasasa misitu inachangia asilimia 75% ya mapato katika mkoa wetu”, amesema Queen Sendiga.

Kongamano hili linatarajiwa kuwaleta pamoja wadau wa sekta ya misitu kutoka ndani na nje ya nchi pamoja na sekta zinazotoa huduma kwenye misitu, wawekezaji wa sekta ya misitu, watunga sera, taasisi na wizara zinazohusika na misitu na uwekezaji (OR TAMISEMI, Wizara ya Maliasiri na Utalii, Wizara ya Uwekezaji, wizara ya viwanda na biashara, kituo cha uwekezaji – TIC,) wazalishaji na wasambazaji wa teknolojia za uchakataji wa mazao ya misitu, taasisi za elimu ya misitu, wadau katika usafirishaji, taasisi za fedha, pamoja na wadau mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa sekta ya misitu
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Queen Sendiga akizungumza wakati wa uzinduzi wa maandalizi ya kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya misitu. Kushoto kwake  ni Mkuu wa willaya ya Kilolo Mh Peres Magiri na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Itinga Mjini Mohamed Moyo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh Queen Sendiga akizungumza baada wa kuzindua  maandalizi ya kongamano la uwekezaji kwenye sekta ya misitu. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mh Saady Mtambule , Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Itinga Mjini Mohamed Moyo na kushoto kwa Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mh Peres Magiri

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...